Leo
Aprili 23,mwaka huu Rais wa Awamu ya Sita, Samia Suluhu Hassan
analihutubia Taifa kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano jijini Dodoma.
Mwandishi
Diramakini amekuwa akikumbana na maswali ya mara kadhaa juu ya iwapo
Rais Samia ni wa Awamu ya Tano au Sita, jibu la jumla ni kwamba ni Rais
wa Awamu ya Sita.
Hii
ni kutokana na ukweli kwamba baada ya kuapishwa Machi 19,mwaka huu
kutokana na kifo cha mtangulizi wake, Hayati Dkt.John Pombe Magufuli
Machi 17, mwaka huu akiwa katika matibabu Hospitali ya Mzena jijini Dar
es Salaam, Rais Samia alianza majukumu yake rasmi.
Hivyo,
baada ya kuapishwa alikuwa na jukumu moja tu la kuhakikisha Taifa
linasonga mbele ikiwemo kutekeleza ahadi zilizoainishwa katika Ilani ya
Uchunguzi ya CCM 2020-2021 kadri anavyoona inafaa ili ilete matokeo ya
haraka.
Hii
ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo tangu aapishwe huku hoja kubwa
ikiwa watu wengi wanajiuliza ni nini hasa Rais Samia atawaambia
Watanzania na Dunia nzima kwa ujumla leo katika hotuba yake hiyo
inayosubiriwa kwa shauku. Tutajuzana hapa, endelea kufuatilia
Tags
Habari