Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeondoa zuio la kampuni za simu nchini kuwatumia mawakala kusajili laini za simu mitaani, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Akizungumza leo Aprili 14, 2021 Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Dkt. Jabir Bakari amesema, mamlaka hiyo imeondoa zuio hilo na sasa kampuni za simu zitaendelea kuwatumia mawakala kufanya usajili.
Zuio hilo lilitolewa Februari 16, 2021 na utekelezaji wake ulitakiwa kuanza Mei Mosi, 2021 ambapo usajili wa laini ulitakiwa kufanyika kwenye maduka ya kampuni husika.
Zuio hilo lilitolewa Februari 16, 2021 na utekelezaji wake ulitakiwa kuanza Mei Mosi, 2021 ambapo usajili wa laini ulitakiwa kufanyika kwenye maduka ya kampuni husika.