TMA yatoa tahadhari kuhusu Kimbunga Jopo Bahari ya Hindi

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inatoa taarifa kuhusu kimbunga Jobo" kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Kumejitokeza mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga hafifu kwa jina Jobo. Kimbunga hicho kipo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi na Mtwara.

Aidha, uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi hususan katika Pwani ya mwambao wa mikoa ya Mtwara na Lindi.

Mamlaka inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na kimbunga hicho ambayo inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa kimbunga Jobo katika wakati ujao.

Wananchi waendelee kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika. Mamlaka ya Hali ya Hewa itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news