Tume ya Utumishi wa Umma itafanya Mkutano wa Tatu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ulioahirishwa tarehe 18 Machi, 2021 kutoa nafasi ya ushiriki katika maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, anaripoti Mwandishi DIRAMAKINI.
Kaimu Katibu wa Tume, Bw. John Mbisso (katikati) akifafanua jambo wakati wa Mkutano wa Tume, kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana na kulia ni Mheshimiwa Balozi (Mstaafu) Bw. John Haule. (Picha na Maktaba-PSC).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bw. John Mbisso, Mkutano huu utaongozwa na Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Jaji (Mst.) Dkt. Steven J. Bwana na utafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 12 hadi tarehe 23 Aprili 2021,Dar es Salaam.
Shughuli zitakazofanyika wakati wa Mkutano huu ni kupokea, kujadili na kutolea uamuzi Rufaa na Malalamiko yaliyowasilishwa na Watumishi mbalimbali wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka zao za Nidhamu.
Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma Mheshimiwa Jaji (Mstaafu) Dkt. Steven J. Bwana akisaini nyaraka wakati wa Mkutano wa Tume ya Utumishi wa Umma hivi karibuni, Mkutano huu utaendelea kufanyika tarehe 12 Aprili 2021 Jijini Dar es Salaam. (Picha na PSC).
Tume ya Utumishi wa Umma inatekeleza majukumu haya kwa mujibu wa Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298
Tags
Habari