Raia hawa wanarudi na ujuzi walioupata huko nje wa kuendesha biashara, kampuni, viwanda, pia wanakuja na uzoefu wao katika kulipa kodi maana huko nje hakuna mianya mingi ya ukwepaji kodi hivyo kwao suala la kodi ni suala la maisha ya kila raia.
Tazama live hapa chini
Wakati hayo yakijiri, Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry, Dk. Charles Gadi amemuomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kusaidia upatikanaji wa uraia pacha kwa raia wa Tanzania wanaoishi nchini na kufanya kazi nje ya nchi.
Askofu wa Kanisa la Good News For All Ministry, Dk. Charles Gadi.
Ombi hilo amelitoa Aprili 21, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema uraia pacha ni muhimu kwani utawawezesha raia waishio nje ya nchi (wanadiaspora) kuwa sehemu ya kuijenga nchi yao kwa kuwekeza mapato yao hapa nchini.
Amesema wakati wa serikali ya Awamu ya nne, Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete aliwashawishi watanzania waishio nje ya nchi kurudi kuja kuwekeza nchini.
Amesema wengi wao walirejea na kununua ardhi na majumba kadhaa, ikiwemo kuanzisha miradi ya kimkakati ya kimaendeleo lakini ghafla ndoto zao ziliimwa kutokana kuzuuliwa kutowekeza katika maeneo waliyoyachukua.
“Jambo hilo lilifanya baadhi yao kupotea mali zao, au kuhamisha majina na kuweka majina ya ndugu zao ili kuepuka kupoteza mali hizo, yakiwemo majumba, mashamba, ardhi na viwanja.
Askofu Gadi amesema raia waishio nje ya nchi wengi wao baada ya kufanya kazi huko kwa muda mrefu, wanatamani kurudi nchini kumalizia pensheni ya uzee wao hapa.
“Raia hawa wanarudi na ujuzi walioupata huko nje wa kuendesha biashara, kampuni, viwanda, pia wanakuja na uzoefu wao katika kulipa kodi maana huko nje hakuna mianya mingi ya ukwepaji kodi hivyo kwao swala la kodi ni swala la maisha ya kila raia.Soma zaidi hapa
Tags
Kimataifa