Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) amewataka Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotumika kusimamia taasisi hizo na si kuwa kikwazo katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika kikao kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Dkt John Mduma akitoa maoni kuhusu ukamilishaji wa mapitio mbalimbali ya Sera na Sheria zinazosimamia taasisi zilizopo chini ya Wizara ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na wakuu wa taasisi hizo kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Waziri Mkumbo aliyasema hayo alipokuwa akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kikao na Wakuu wa Taasisi hizo kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
“Taasisi zote zilizochini ya Wizara ya Viwanda zinamchango mkubwa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara hivyo nawasihi muendelee kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria Kanuni na taratibu zinazosimamia taasisi zenu katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi na si kuwa kikwazo,"amesema.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji akitoa maoni kuhusu uboreshaji wa huduma zinazotolewa na SIDO kwa Mhe. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Bw. Dotto James akifafanua jambo katika Kikao cha Wizara na Wakuu wa Taasisi zake Kikao hicho kilicholenga kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara kilifanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (Mb) akitoa mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara alipokutana na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara katika kikao kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Aidha, Wakuu wa Taasisi waliohudhuria kikao hicho kutoka TBS, WMA, BRELA, TANTRADE, SIDO, NDC, EPZA, FCC, FCT, WRRB, TIRDO, CAMARTEC, TEMDO na CBE walipata fursa ya kutoa maoni na changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake kwa Mhe.Waziri wa Viwanda na Biashara.
Waziri Mkumbo ameahidi kuendelea kupokea ushauri wa kitaalamu kutoka katika taasisi hizo pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili taasisi hizo katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwemo upatikanaji Bodi zinazofanya kazi katika kila taasisi ili kurahisisha utoaji wa maamuzi sahihi na kwa wakati.
Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bi. Stella Kahwa, Katikati ni Mrajis wa Baraza la Ushindani Bw Renatus Rutatinisiwa akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu waa NDC Bi Rhobi Sattima wasilikiliza maelekezo ya Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo katika kikao na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara kilichofanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) (kulia) akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah (kushoto) wakiwa katika Kikao cha Wizara na Wakuu wa Taasisi zake. Kikao hicho kilicholenga kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Wizara kilifanyika tarehe 09/04/2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara jijini Dodoma.
Naye Naibu Waziri akiongea na Wakuu wa Taasisi hizo, alisema kuwa mchango wa taasisi hizo ni muhimu na zinategemewa katika kuifanikisha Wizara kufikia malengo ya taifa katika ukuaji wa viwanda na biashara shindani na hivyo kukuza uchumi wa nchi.