Waziri Ummy aziweka mtegoni shule zitakazofanya udanganyifu wa mitihani

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa shule za umma na binafasi kutojihusisha na udanganyifu na uwizi wa mitihani,anaripoti Angela Msimbira (TAMISEMI).
Akifunga kikao kazi kilichowakutanisha Maafisa elimu Kata Tanzania Bara leo Jijini Dodoma Waziri Ummy amesema tabia ya udanganyifu na uwizi wa mitihani ni jambo ambalo linatia aibu taifa na kuwa si msingi mzuri wa kuwajenga watoto.

“Tunashukuru serikali imeweza kuimarisha usimamizi wa mitihani, lakini bado kunaudanganyifu kwenye mithani hali ambayo inatia aibu na doa serikali yetu na madhara yake ni makubwa.amesisistiza Waziri Ummy.

Amemuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Profesa. Riziki Shemdoe kuangalia mfumo mzuri wa kuwapima waalimu katika uwajibikaji wao kwa kuwa zipo sababu zinazochangia mwananfunzi kutokufanya vizuri darasani.

“Suala la kuwa shule ikifanya vibaya basi walimu wakuu, afisa elimu wanachukuliwa hatua na kushushwa vyeo, na hili pia linachangia wimbi la udanganyifu na uwizi wa mitihani, hivyo katibu mkuu kuna haja ya kuja na vipimo vya kuwapima kama wamewajibika kiasi gani, kwani wakati mwingine shule kufanya vibaya watu hawa hawahusiki moja kwa moja,"amesema.
Waziri Ummy amemuagiza Kaibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuwaandikia barua wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga bajeti kwa ajili ya mafuta na matengenezo ya pikipiki za maafisa elimu kata ili waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Aidha, amewataka maafisa elimu kata kuhakikisha wanasimamia kwa karibu utekeleza wa ujenzi wa miundombinu na kuwa kwa kufanya hivyo wataweza kutimiza agizo la Rais Samia la kutotaka kuona mtoto wa kitanzania akisoma chini ya mti na kukaa chini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news