YouTube yasimamisha TV mtandao wa TB Joshua kwa kuwaponya watu wa mapenzi ya jinsia moja

YouTube imesimamisha akaunti ya mhubiri maarufu wa Televisheni wa Nigeria TB Joshua juu ya madai ya matamshi ya chuki.
Kwa mujibu wa BBC, shirika moja la kutetea haki liliwasilisha lalamiko baada ya kukagua video zisizopungua saba zikimuonesha mhubiri huyo akifanya maombi ya kuwaponya watu wa mapenzi ya jinsia moja

Facebook pia imeondoa moja ya machapisho ambayo yanaonesha mwanamke akipigwa kofi wakati TB Joshua akimuombea na kusema anatoa "roho ya pepo".

Mhubiri huyo alisema alikuwa akikata rufaa dhidi ya uamuzi wa YouTube.

TB Joshua ni mmoja wa wainjilisti wenye ushawishi mkubwa barani Afrika, na wanasiasa wakuu kutoka bara zima ni miongoni mwa wafuasi wake.

Kwanini akaunti yake imefungwa ?

Shirika la Open Democracy lenye makao yake nchini Uingereza liliwasilisha malalamiko baada ya kukagua video saba zilizochapishwa kwenye idhaa ya YouTube ya TB Joshua Ministries kati ya 2016 na 2020, ambayo inaonysha kuwa mhubiri huyo anafanya maombi "kuponya" watu wa mapenzi ya jinsia moja.

Msemaji wa YouTube aliiambia OpenDemocracy kwamba akaunti hiyo ilifungwa kwa sababu sera yake "inakataza maudhui ambayo yanadai kwamba mtu ni mgonjwa wa kiakili, anaugua, au ni duni kwa sababu ya ushirika wao katika kikundi kinacholindwa pamoja na mwelekeo wa kijinsia".

Ujumbe kwenye akaunti ya Facebook ya TB Joshua Ministries uilisema: "Tumekuwa na uhusiano mrefu na wenye mafanikio na YouTube na tunaamini uamuzi huu umefanywa kwa haraka."

Video hiyo inaonyesha nini?

Video hiyo ni ya kipindi cha maombi cha mwanamke anayeitwa Okoye, iliyopeperushwa kwanza mnamo 2018.

Ndani yake TB Joshua anampiga makofi na kumsukuma Okoye na mwanamke asiyejulikana kama mara 16 hivi na kumwambia Okoye: "Kuna roho inakusumbua imejipandikiza ndani yako. Ni roho ya mwanamke," openDemocracy inaripoti.

Video hiyo ambayo ilitazamwa zaidi ya mara milioni 1.5 kabla ya akaunti ya YouTube kuishusha, baadaye inamuonesha akishuhudia mbele ya mkutano kwamba "roho ya mwanamke" ilikuwa ikiharibu maisha yake lakini alikuwa ameponywa baada ya maombi ya muhubiri huyo.

Anatangaza kwamba alikuwa ameacha kuwa na "mapenzi" kwa wanawake na "sasa nina mapenzi kwa wanaume".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news