Brela yawataka wabunifu kusajili bunifu zao

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela)imewataka wabunifu na Wavumbuzi wa Sayansi na Teknoloijia kwenda Brela kusajili bunifu zao ili kuzipa ulinzi na kulindwa kisheria.
Afisa Mwandamizi- Utumishi na Utawala kutoka Idara ya Miliki Ubunifu BRELA, Bw.Raphael Mtalima akifafanua juu ya sifa za Uvumbuzi unaoweza kusajiliwa kama Hataza kupitia BRELA wakati wa mashindano ya MAKISATU yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma leo. BRELA inawakaribisha kutembelea kwenye banda lake katika mashindano ya MAKISATU yaliyoanza tarehe 6 hadi 11 Mei, 202

Aidha, Brela pia imewataka wabunifu hao kurasimisha Biashara zao ili waingie katika mfumo rasmi wa kutambulika Kitaifa na Kimataifa.

Hayo yalisemwa na Afisa Utumishi na Utawala anayehusika na maombi ya Ataza,Alama za Biashara na Huduma BRELA, Bw. Raphael Mtalima katika maonesho ya Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Bunifu (MAKISATU) yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Jijini hapa.

"Niwatake Hawa wabunifu na wavumbuzi walinde vumbuzi zao kwa kuzisajili Brela, hii itamsaidia kutambulika ndani na nje hata akiitaji mkopo kwaajili ya kuendeleza Biashara yake inakuwa rahisi,"amesema Afisa Mtalima.

Aidha, Mtalima aliongeza kuwa vumbuzi,bunifu na teknolojia mbalimbali za Kisayansi Brela ndio Taasisi inayosismamia Sheria ya Ataza, alama za Biashara na huduma hivyo inawajibu wa kutoa kwa wajasiriamali.

"Lazima wabunifu hawa wafaidike na Bunifu zao kwani wanatumia pesa nyingi kufanya tafiti zao hivyo ili kuweka Ulinzi wa hizo Bunifu zao ikiwa ni njia Kuu za kuwafaidisha kisheria,"amesema Mtalima.

Aidha, Afisa huyo wa Brela pia amewataka wakazi wa Dodoma na vitongoji vyake kutumia maonesho hayo kwenda kusajili Biashara zao kwani huduma zinapatikana hapo hapo uwanjani.

Vilevile Mtalema alisema kuwa huduma za Brela pia zinapatikana kwa njia ya mtandao hivyo popote Tanzania huduma hizo zinapatikana.

Mashindano na maonesho hayo ya MAKISATU yaliyoanza Mei 6 hadi 11 mwaka huu na yamejumuisha zaidi ya wabunifu 100.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news