Mjasiriamali maarufu Carol Ndosi ameeleza kuwa, yeye ni miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mazingira mazuri kwa Wawekezaji yaliyopo nchini Tanzania yanayotengenezwa na Serikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ambayo yamefanya yeye kuweza kujiajiri na kufanya kazi zake kwa urahisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.(Picha na Ikulu/Diramakini Blog).
Carol Ndosi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema yeye amejiajiri kwa kuandaa na kuratibu Matamasha makubwa ya NyamaChoma na ameweza kufanya hivyo kutokana na mazingira rafiki ya Kibiashara yaliyopo Tanzania kwa sasa.
Carol amesema, haoni sababu ya watu kuilaumu Serikali kuhusu suala la ajira badala yake waipongeze Serikali ya Awamu ya Sita kwa mazingira mazuri inayotengeneza ili Sekta Binafsi zizalishe ajira nyingi.
"Mimi siilaumu Serikali kwamba imeshindwa kutengeneza ajira kwa sababu sio Mwajiri mkuu pekee, Serikali inatengeneze mazingira kwa Sekta binafsi kutengeneza fursa na vijana kujiajiri," amesema Carol Ndosi.
Alichokisema Mjasiriamali Carol Ndosi kimeakisi hatua nzuri anazoziendea Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan hasa kwenye kuweka mazingira mazuri ya watu kupata ajira kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020- 2025 kwa kuanza kuwavutia Wawekezaji wa ndani akiwemo Carol Ndosi pamoja na waliopo nje ya nchi.
Tags
Habari