Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii wameendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaopakana na hifadhi za wanyama, mapori ya akiba jinsi ya kupambana na wanyama waharibifu ikiwemo Tembo,anaripoti Derick Milton (Meatu).
Vijana waliopata mafunzo wakifunga vitambaa venye pilipili, kwenye moja ya mashamba lilipo katika wilaya ya Maetu ambalo linadaiwa kuvamiwa na tembo ambao utokea katika pori la akiba la Maswa.
Taasisi hiyo imeendelea kufundisha wananchi hao mbinu mbalimbali za kupambana na wanyama hao bila ya kuwadhuru, ambapo moja ya njia hizo ni matumizi ya kondomu za kiume.
Akiongea mara baada ya mafunzo kwa vijana 30 kutoka Wilaya za Itilima, Meatu na Bariadi ambazo zinapakana na pori la akiba la Maswa Mkoani Simiyu Kaimu Mkurugenzi wa taasisi hiyo Dkt. Janemary Ntalwila alisema kuwa kondomu hizo zinatumika kutengeneza mabomu ya kufukuza tembo.
Wakuu wa Wilaya za Itilima, Meatu na Bariadi Mkoani Simiyu, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) Jinsi ya kutumia mabomu ya mishumaa wakati wa kufukuza tembo au wanyama wanaovamia mashamba ya wananchi (Picha na Derick Milton).
Alisema kuwa, licha ya vijana hao kufundishwa njia nne za kupambana na tembo ambao ndiyo wananyama wasumbufu, njia hiyo ya kutumia mipira hiyo ya kiume ni rahisi kutengenezwa na kupatikana.
Alisema kuwa njia nyingine ambao wamefundishwa vijana hao ni ufungaji wa nyuki kwenye mashamba, ufungaji wa uzi wenye pilipili kuzungushia mashamba, pamoja na utengenezaji wa tofali lenye pilipili.
Wakuu wa Wilaya za Itilima, Meatu na Bariadi Mkoani Simiyu, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) Jinsi ya kutumia mabomu ya mishumaa wakati wa kufukuza tembo au wanyama wanaovamia mashamba ya wananchi (Picha na Derick Milton).
Amesema, njia nyingine ambazo walifundishwa vijana hao ni matumizi ya mabomu ya mishumaa, pamoja na matumizi ya mambomu yaliyotengenezwa kwa kondomu za kiume.
Alisema kuwa njia zote hizo zimekuwa zikileta manufaa, huku akibainisha kuwa endapo wanyama wamegoma kuondoka kwenye mashamba ya wananchi, ndipo njia za mabomu hayo zinaruhusiwa kutumika.
Vijana waliopata mafunzo wakiwa wameshikilia mabomu yalitengenezwa kwa kutumia Kondomu za kiume, wakiwa tayari kurusha juu kuonyesha jinsi ya kufukuza tembo
“ Ile mishumaa ya mambomu gharama zake ni kubwa sana kuipata, kila mmoja ni zaidi ya shilingi 30,000, na ndani mwake kuna mabomu 5 na ndiyo njia ya haraka kuweza kufukuza tembo, lakini taasisi yetu iliona kuja na njia nzuri ya mambomu ambayo wananchi wengi wataimudu,” alisema Dkt Ntalwila
“ kutokana na mabomu ya mishumaa kuhitaji gharama kubwa, tuliona njia hii ya matumizi ya kondomu ndiyo njia rahisi kupatikana kwa wananchi wetu na wanaweza kutengeneza wenyewe muda wowote,” aliongeza Dkt Ntalwila.
Juma Nasoro mmoja wa vijana waliopewa mafunzo hayo, alisema kuwa katika utengenezaji wa mabomu ya mipira hiyo, uwekewa pilipili, mchanga pamoja na kilipuzi, na baadaye kurushwa juu na kuripuka,” alisema Juma.
Wakuu wa Wilaya za Itilima, Meatu na Bariadi Mkoani Simiyu, wakipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Taasisi ya utafiti wa wanyamapori (TAWIRI) Jinsi ya kutumia mabomu ya mishumaa wakati wa kufukuza tembo au wanyama wanaovamia mashamba ya wananchi (Picha na Derick Milton)
“Unaporusha juu ule mlio au sauti ya bomu pamoja na pilipili vinamkimbiza tembo, maana ni myama ambaye hapendi kelele wala muwasho, njia nyingine ni mwanga wa tochi lakini pia kelele za mavuvuzela,” alieleza Juma.
Kwa upande wake Afisa Wanyamapori mkuu Wizara ya Maliasili na utalii Pellage Kauzeni alisema kuwa serikali itaendelea kuibua mikakati mbalimbali kila mara kwa kushirikiana na wadau wa utalii katika kupambana na wanyama waharibifu.
Kauzeni alisema kuwa mbali na elimu, serikali imeendelea kutoa kifuta machozi na kifuta jasho licha ya kuchelewa kutokana na utaratibu wa kifedha uliopo, ambapo alieleza wameanza kulipa baadhi ya watu ambao waliadhirika na wanyama.
“Tunajua watu wanaongea hasa katika njia hii ya matumizi ya Kondomu, lakini hii ndiyo njia rahisi na sahihi kwa wananchi wetu, waweze kupambana na wanyama hao na sisi kama serikali tutaendelea kutoa elimu hii kwa wan anchi wote ambao wanapakana na hifadhi,” alisema Pellage.
Ufungwaji wa mafunzo hayo ilihudhuriwa na wakuu wa Wilaya hizo ambao walionyeshwa jinsi ya utemngenezwaji wake, na Mkuu wa Wilaya ya Meatu Dkt Joseph Chilonganyi aliitaka Wizara kusaidia upatikanaji wa vifaa kwa wananchi hasa pale wanapovamiwa na tembo.
Tags
Habari