Wekundu wa msimbazi Simba SC wamepoteza mchezo wake wa ugenini wa mashindano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kupokea kipigo cha mabao 4-0 kutoka timu ya Kaizer Chiefs ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa hatua ya robo fainali katika Dimba la FNB jijini Johannesburg Afrika Kusini.
Mlinzi wa kati wa Kaizer Chiefs Eric Mathoho aliipatia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya 6 ya mchezo huo, huku Samir Nurkovic akipachika mabao mawili katika dakika ya 34 na 57 ya mchezo huo ambapo David Leonardo Castro Cortés akipigikia msumari wa mwisho na kuongeza goli la nne Katika dakika ya 63 ya mchezo huo.
Mchezo wa marudiano utafanyika Jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi ijayo tarehe 22 ambapo Simba SC watahitajika kushinda mabao 5-0 ili kuweza kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Mchezo | Kaizer Chiefs vs Simba SC |
Tarehe | Jumamosi, Mei 15 |
Muda | 18:00 SA/ 7:00 Tz |