CHAMA cha ACT Wazalendo kimempoteza Mbunge wake kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Khatib Said Haji kutoka Jimbo la Konde kisiwani Pemba.
Kutokana na uwepo wa mahabusu hao kwa muda mrefu gerezani Tanzania Bara aliomba Serikali ifanye uamuzi wa busara ili kuona wanapewa haki ya kuachiwa huru.
Kifo cha Mheshimiwa Haji kimethibitishwa na Katibu Idara ya Bunge Baraza la Wawakilishi na Serikali za Mitaa, Hamad Yussuf leo Mei 20, 2021.
"Nasikitika kuwatangazia Kifo Cha Mhe Khatib Said Haji Mbunge wa Jimbo la Konde, ambaye umauti umemfika akiwa anapatiwa Matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Alfajiri ya leo, mipango ya mazishi inaendelea na tutajulishwa baadae kidogo.
Akichangia
bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 alisema ,
matokeo ya hilo nyumbani kwake kuna watu wawili amewaambukiza na huko
hospitali haijulikani matokeo yake nini.
“Ndani ya siku tatu ameng’ang’ana kukaa hospitali ya Mnazi Mmoja matokeo yake akatolewa kwa nguvu baada ya kuona jambo hili limekuwa kubwa sana. Baada ya malalamiko makubwa ndio alikubali kuwekwa kwenye karantini,”aLIsema Haji wakati wa uhai wake.
ALIsema alifanya hivyo kwa sababu ya kiburi cha madaraka yake na kumpongeza makamu wa pilli wa Rais Zanzibar wakati huo kabla ya Serikali ya Awamu ya Nane kwa kukubali kukaa karantini alipotoka nje ya nchi bila kulazimishwa.
“Huu ndio utu, huu ndio ubinadamu leo
waziri huyu ni nani anayekataa uamuzi wa Serikali hata uamuzi wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.Hatuwezi kumchekea mtu mheshimiwa
Waziri Mkuu kwa sababu ni waziri ulichukulie hatua haraka. Leo hii baada
ya kiburi kingine kuna mtu mwingine ni daktari anaitwa Hafidh hadi leo
ameng'ang'ana pale Hospitali ya Mnazi mmoja kwa sababu ana unasaba wa
kiukubwa.
“Uheshimiwa wake ni kwa sababu ana uhai anapumua dakika moja akifumba macho anakuwa marehemu. Taharuki iliyopo pale Mnazi mmoja baada ya matukio hayo ni kubwa. Nataka mheshimiwa ufuatilie kama huyu daktari bado yupo,”alisema.
Mheshimiwa Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF
mwaka 2010 hadi 2020. Pia alishawahi kushika nafasi ya Waziri wa Kilimo
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1984 hadi 1987.
Katika Bunge hili la 12, Khatib amekuwa Mbunge wa tatu kufariki tangu
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. Januari 21, 2021 Mbunge wa Viti Maalum
(CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla alifariki dunia na Februari 12, 2021 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Atashata Nditiye alifariki dunia baada ya kupata ajali ya gari mkoani Dodoma.
WASIFU WA MHESHIMIWA KHATIB SAID HAJI KABLA YA KUJIUNGA ACT WAZALENDO UCHAGUZI WA MWAKA 2020.
Hon. Khatib Said Haji
Member Type : Constituent Member
Constituent : Konde
Date of Birth : 1962-07-31
Education History :
School Name/Location | Course/Degree/Award | From | To | Level |
---|---|---|---|---|
Konde Secondary School | - | 0 | 0 | Secondary School |
Utaani Secondary School | CSEE | 0 | 0 | Secondary School |
Micheweni Primary School | CPEE | 0 | 0 | Primary School |
Employment History :
Company/Institution | Position | From | To |
---|---|---|---|
Ministry of Agriculture (SMZ) | Pay Master/Accounts | 1984 | 1987 |
Political Experience :
Political Party | Position | From | To |
---|---|---|---|
Economic Affairs, industries and Trade Committee | Member of Committee | 2010 | 2015 |
Parliament of Tanzania | Member of Parliament | 2015 | 2020 |
Parliament of Tanzania | Member of Parliament | 2010 | 2015 |
Civic United Front (CUF) | Member of District Committee | 1995 | 1995 |
Industries, Trade and Enviroment Committee | Member | 2015 | 2018 |