MRATIBU KITAIFA WA MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA AFANYA ZIARA MKOA WA SHINYANGA

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, Wakili Onesmo Olengurumwa akiambatana na Afisa Ushawishi na Wanachama, Bi. Lisa Kagaruki, wameendelea kutembelea Shirika la The Voice of Marginalized Community (TVMC), Shinyanga mjini.
TVMC ni taasisi inayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu kupitia programu zifuatazo; Utoaji wa Msaada wa Kisheria kwa wanawake, watoto na makundi maalum, Ulinzi na Usalama wa Mtoto, Utetezi wa Ukatili wa kijinsia.

Shirika hili limejikita kufanya kazi nchi mkoa mzima wa Shinyanga ikishirikiana na mashirika mbalimbali mkoani humo na Tanzania nzima yakiwemo Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS). TVMC hushirikiana na TLS katika kesi mbalimbali za kimkakati.

Pamoja na Kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na TVMC, bado kumekuwa na changamoto mbali mbali ambazo shirika hili limekuwa likikutana nazo ambazo ni pamoja na;

-Mtazamo hasi kutoka kwa jamii inayowazunguka, juu ya utetezi wa haki za mtoto na mwanamke. Mkoa wa Shinyanga ni mkoa wenye mfumo dume. Hivyo basi ni ngumu kwa jamii kuelewa kwanini mtu hujitokeza ili kutetea haki za mwanamke.

-Ukosefu wa nyumba salama kwa ajili ya wahanga wa ukatili wa kijinsia. Hii changamoto ni kubwa sana, ambapo kama mhanga huyu akiendelea kuishi eneo ambalo ndilo alilopata ukatili, kuna uwezekano mkubwa wa kutokupata haki yake. Hii ni kwasababu ya ushawishi mbaya kutoka kwa jamii inayomzunguka.

-Rushwa kuanzia ngazi ya chini ya uongozi. Baadhi ya maafisa wa serikali hasa askari polisi, wanasemekana kutokua waaminifu na kusababisha kuwavunja moyo watetezi wa haki za binadamu.

Pamoja na Changamoto hizo, kumekuwa na faida mbalimbali ikiwemo;
 
-Mahusiano mazuri na serikali za ngazi zote, ambapo kuna wakati ambapo serikali wanakua mstari wa mbele katika utetezi.
 
-TVMC inashirikiana vyema na mashirika mengine ikiwemo TLS na Agape Aids Control Program.

Baada ya kuskiliza changamoto na fursa za taasisi ya TVMC, Mratibu wa Mtandao ameipongeza sana na amelishauri shirika hilo kuendelea na mashirikiano mema na serikali.

Ameshauri pia kuwepo na mshikamano kati ya wanachama wa Mtandao, hasahasa wanaotetea haki ya aina moja. TVMC inaweza kuishika mkono Agape Aids Control na kusaidiana nao katika kujenga safe-house nzuri kwa wahanga.

Afisa dawati ameendelea kusisitiza TVMC kuwasiliana na watetezi TV katika kuibua uvunjifu wa amani unaoendelea mkoani humo. Mnamo mwaka 2020, TVMC ilikua mstari wa mbele kutaarifu Mtandao na Watetezi TV juu ya uvunjifu unaoendelea mkoani humo. Yawapasa kuendelea na mwendo huohuo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news