MWALIMU MAKURU LAMECK AHIMIZA SERIKALI KUSHUGHULIKIA HARAKA SUALA LA ELIMU KUNUSURU SEKTA BINAFSI

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeombwa kuzifanyia mabadiliko sheria kandamizi katika sekta hiyo pamoja na kulitazama kwa kina suala la wanafunzi wanaohitimu darasa la saba, kidato cha nne na kutoruhusiwa kurudia, kwani kufanya hivyo ni kuchangia Taifa likose Wasomi watakaoliletea maendeleo katika nyanja mbalimbali, anaripoti Amos Lufungilo (Diramakini) Mara.
Ombi hilo limetolewa na Kada wa CCM Wilaya ya Musoma Mjini,  Mwalimu Makuru Lameck Joseph wakati akiongea na Diramakini Mjini Musoma. 

Ambapo amesema, miongoni mwa mambo ya msingi yanayopaswa kutazamwa na Serikali ni pamoja usajili hususan mtoto anapofeli, sheria hazimpi mtoto fursa ya kurudia shule akiwa katika mfumo rasmi, badala yake humfanya atumie mfumo usio rasmi wa kujitegemea kidato cha nne na cha sita ambao si rafiki.

Amesema kuwa, jambo hilo humnyima Mtoto fursa ya kusoma katika mtaala rasmi kulingana na umri mdogo kwani baadhi yao hufeli kwa bahati mbaya na wengine kutokana na umri wao kuwa mdogo, kwani hushindwa kujitambua wawapo shuleni. 

Jambo ambalo huchagizwa na baadhi yao kuanza masomo wakiwa na umri mdogo na kutotilia maanani suala la elimu kwa wakati huo wakiwa shuleni.

Ameongeza kuwa, kutokana na hali hiyo wanapojitambua na kutaka kurudi katika masomo hujikuta hawawezi kupata fursa hiyo kutokana na sheria kutoruhusu kurudia shule kwa darasa la saba, kidato cha nne na cha sita. 

Na hivyo kuwafanya wakose fursa ya kupata elimu kutokana na sheria kandamizi katika mfumo wa elimu uliopo kwa sasa.

Aidha, ameishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuzipitia sheria zake upya na kuona namna bora ya kuzifanyia marekebisho ili Watoto hao waweze kupata nafasi ya kurudia kwa uhuru na haki. 

Jambo ambalo litawafanya wapate elimu ya kutosha, maarifa na ujuzi kwa ajili ya maisha yao kwa siku za usoni na Taifa kwa ujumla.

Pia, ameomba serikali iweze kuzipa shule Binafsi Nchini ridhaa ya kusajili Wanafunzi katika mfumo rasmi wa masomo kwa watakaotaka kurudia ama kiendelea na masomo pindi wanapokuwa wameshindwa kuendelea na masomo katika Shule za Serikali na Binafsi wapewe fursa hiyo bila kizuizi.

"Shule Binafsi zinapotaka kusajili Wanafunzi waliohitimu na kufeli darasa la Saba, kidato cha nne na cha sita mfumo wa usajili hukataa kuwasajili na huonesha kwamba wamekwisha soma awali na hivyo huwanyima fursa ya kurudia shule na kupata elimu ambayo ni haki ya Msingi kwa kila mtanzania kwa manufaa yake na Taifa letu.

"Jambo hili limefanya shule nyingi za binafsi pamoja na vyuo vingi kufungwa kutokana na kukosa wanafunzi. Hili linatokana na sheria kandamizi zilizowekwa na Wizara ya Elimu ambazo zimekuwa si rafiki hususani katika upande wa urudiaji Wanafunzi haziruhusu. Zimeweka sheria ngumu kutoruhusu kurudia shule. Hivyo huwanyima fursa Wazazi ambao Watoto wao wanapofeli hutaka kuwaendeleza katika Shule binafsi hali ambayo inaweza kuongeza idadi kubwa ya watu wasioelimka,"amesema Mwalimu Makuru.

"Kutokana na sheria kutoruhusu wanafunzi kurudia shule, imechangia watu kutumia majina ya watu wengine yasiyo ya kwao. Hivyo huleta migogoro katika Jamii pindi wanaposikia mtu katika Jamii ikiitwa jina lisilo lake na mwenye nalo yupo kijijini/ Mjini huku akiwa hana kazi yabkufanya na aliyetumia jina hilo ana kazi Serikalini ama sekta Binafsi na hivyo huongeza chuki na uhasama katika Jamii,"ameongeza.

Ameongeza Kuwa, kipindi cha nyuma sekta binafsi hususan katika sekta ya elimu ilisaidia Sana Serikali kwa kuchukua idadi kubwa ya Wanafunzi kuanzia shule za Msingi na vyuo vya Kati na vyuo Vikuu. Hii ilitokana na serikali kuandaa Mazingira mazuri na rafiki ya kupata fursa kubwa kwa shule binafsi na vyuo kusajili Wanafunzi wengi tofauti na miaka ya hivi karibuni. 

Ambapo Taasisi nyingi za Binafsi upande wa elimu zimedhorota na zingine kufungwa na hata kufa.

Aidha, amesema kutokana na hali hiyo. Wadau wengi wa elimu hususan shule binafsi na vyuo wamejikuta wakiilalamikia Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua madhubuti za makusudi za kunusuru sekta hiyo.

Ambayo pia hutoa mchango mkubwa wa Maendeleo ya uchumi, Kijamii, kisiasa na kitamaduni kwa kuajiri Walimu wengi waliokuwa wakihitimu katika vyuo vingi Nchini kwa kulipwa mishahara minono.

"Miaka ya 2005 hadi 2015 tuliona shule binafsi na vyuo vilikua na kujengeka kwa Kasi kubwa sana Kutokana na uongozi wa kipindi hicho kuvipa fursa. Sekta binafsi upande wa elimu ni muhimu sana katika Taifa letu husaidia katika mapambano ya maadui watatu katika Taifa letu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini. Niiombe Wizara ya Elimu itambue kuwa elimu ndiyo nguzo ya kuendeleza Nchi katika nyanja zote katika kupambana na maadui hao kwa sekta mbalimbal,"amesema.

Katika hatua nyingine Mwalimu Makuru Lameck Joseph amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kushughulikia matatizo mbalimbali ya Wananchi ikiwemo suala la elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news