Nyota wa Muziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amefanikiwa kufanya Ibada Maalum ya Umrah, Ibada ambayo alishindwa kuitimiza kutokana na maradhi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kupitia Ukurasa wake wa Instagram, #OmmyDimpoz ameshare picha akiwa Maka ambako ameandika ujumbe ambao unaonesha alivyo na furaha kukamilisha jambo hilio Tukufu katika maisha yake.
Umrah ni Ibada ya Sunnah kwa mwenye uwezo, ambayo hufanyika ibada zote ndani ya "makkah" yaani mfano kuswali,kusoma Quran na kuizunguka Al Qabah,kutembelea sehemu takatifu,kaburi la mtume na maswahaba.
Ibada hizi unaweza kufanya siku yoyote lakini watu hupenda kufanya kipindi cha mwezi wa Ramadhani wakiwa na swaumu, wengine karibu na Eid Fitril,
Ibada hizi zinakuwa na uzito na ujira mkubwa sana, utofauti ya Umrah na Hijjah ni kwamba "Hijjah ipo katika nguzo 5 za Uislamu, ambayo ni lazima kwa mwenye uwezo na katika Umrah hakuna Arafa wala hakuna kurusha mawe wala kuchinja mnyama, kwenye Eidd el fitr inakusanya ibada ya Umrah pekee lakini ile ya Idd kubwa (Eid El Haij) ya kuchinja ndiyo inakusanya Umrah na Hajj kwa wale mahujaj ambao wameenda.
Tags
Habari