PROF.MKUMBO ATEMBELEA KITUO CHA WMA MISUGUSUGU MKOANI PWANI

NA EMMANUEL MBATILO, PWANI

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo amesema serikali ina mfumo mzuri wa kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma ambazo zimehakikiwa kupitia Wakala wa Vipimo (WMA) ili wananchi waweze kupata huduma iliyosahihi.
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (Kulia) akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani kuhusu namna zoezi la kuhakiki mita za maji linavyofanyika mara baada ya kutembelea leo Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa Pwani.

Ameyasema hayo leo alipotembelea Kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu Mkoa aa Pwani kuangalia namna shughuli inavyofanyika katika kituo hicho.

Aidha Prof.Mkumbo amewataka wananchi ambao walikuwa na malalamiko ya kubambikiwa bili na mamlaka husika kutumia Kituo hicho kuweza kutatuliwa changamoto zao katika vipimo.

“Kwa wale wananchi ambao wapo karibu na kituo hiki wasisite kutumia kituo hiki lakini kwa nchi nzima ni vizuri wananchi wanapokuwa na wasiwasi watumie vituo vyetu vya wakala ambavyo vipo katika kila Mkoa hapa nchini ili kupata huduma ambazo zimehakikiwa”. Amesema Prof.Mkumbo. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akiambatana na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu (WMA), Bi.Stella Kahwa mara baada ya kuwasili leo katika kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu mkoani Pwani na kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA). Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (wa pili kushoto) akishuhudia uhakiki wa matanki ya magari ya mafuta ukifanyika mara baada ya kuwasili leo katika kituo cha Wakala wa Vipimo (WMA) Misugusugu mkoani Pwani na kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA).

Magari ya mafuta yakihakikiwa matanki Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo (katikati) akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) mara baada ya kufika leo katika Kituo cha (WMA) Misugusugu mkoani Pwani kushuhudia kazi zinazofanywa na (WMA).(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO).

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) mkoa wa Pwani Bw. Alban Kihula wamenunua mtambo wa kuhakiki mita za umeme ambao unaweza kuhakiki mita 20 kwa mara moja ambapo utaanza hivi karibuni.

“Tumeshakaa na wazalishaji wa mita za umeme hapa nchini na zoezi linaloendelea kwa sasa kuhakiki sampuli za mita kabla hazijakwenda kwa wateja”.Amesema Bw.Kihula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news