Rais Samia afanya mazungumzo na Rais mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo katika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma,ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.

Taarifa ya Ikulu imesema, katika mazungumzo hayo, Obasanjo ametoa salamu zake za rambirambi kwa Rais Samia kufuatia vifo vya waliokuwa Marais wa Tanzania Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki Dunia Julai 23, 2020 na Hayati Dkt. John Magufuli aliyefariki Dunia Machi 17, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumzo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma leo. (Picha zote na Ikulu).

Rais Mstaafu Obasanjo amempongeza Rais Samia kwa kupokea kijiti cha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na amemtakia heri katika majukumu yake.
Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, akizungumza na Waandishi, wakati akisindikizwa na mwenyeji wake, Rais Samia, Baada ya nazungumzo yao, leo Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo, wakati akimsindikiza mgeni wake, baada ya mazungumzo yao, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma leo.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao pia wamezungumzia hali ya usalama Barani Afrika na umuhimu wa Wakuu wa Nchi kujadiliana na kutafuta suluhisho la migogoro hiyo ambayo inasababisha vifo vya watu wasio na hatia hasa wanawake na watoto.

Wamezungumzia pia masuala ya maendeleo hasa katika uchumi na kusisitiza umuhimu wa nchi za Afrika kuongeza ushirikiano na kuondoa vikwazo vya biashara na uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news