Na Diramakini (diramakini@gmail.com)
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa mabalozi 23 akiwemo mrembo wa Tanzania mwaka 1999, Bi.Hoyce Temu.

Wengine ni Edwin Rutegaruka, Fredrick Kibuta, Noel Kaganda, Mindi Kasiga, Caroline Chipeta, Macocha Tembele, Agnes Kayola, Masoud Balozi, Ceasar Waitara, Swahiba Mndeme pamoja na Said Mshana.
Pia Rais Samia amewateua Alex Kallua, Mahmoud Kombo, James Bwana, Said Mussa, Elsie Kanza pamoja na Robert Kahendaguza.
“Uteuzi wa Mabalozi hawa umeanza leo Mei 22, 2021 na wataapishwa kwa tarehe zitakazotangazwa baadaye,” imesema taarifa hiyo kama inavyoendelea kusomeka hapa chini;
Tags
Habari