Rais Samia:Msimamo bado haujabadilika

 Kuhusu Tanzania kufuta tamko la kuruhusu taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) na watu binafsi kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika Mahakama hiyo, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania italiangalia jambo hilo lakini kwa sasa msimamo haujabadilika.

Na Mwandishi Diramakini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Mei, 2021 amekutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mhe. Sylvain Ore ambaye anamaliza muda wake tarehe 31 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu (African court on Human and peoples’ Rights) Mhe. Jaji Sylvain Orè mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Mei, 2021.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Rais Samia ameipongeza Mahakama hiyo ambayo makao yake makuu yapo Jijini Arusha, Tanzania kwa kazi inazozifanya na amemhakikishia Mhe. Ore kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutoa ushirikiano ikiwemo kushughulikia changamoto mbalimbali kwa kuwa inatambua umuhimu wa majukumu yake.

Aidha, Mhe. Rais Samia amempongeza Mhe. Ore kwa utumishi wake wa vipindi viwili vya Urais wa Mahakama hiyo na amemuomba kuendelea kuwa balozi mwema wa Tanzania.

Kuhusu Tanzania kufuta tamko la kuruhusu taasisi zisizo za kiserikali (NGOs) na watu binafsi kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika Mahakama hiyo, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania italiangalia jambo hilo lakini kwa sasa msimamo haujabadilika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu (African court on Human and peoples’ Rights) Mhe. Jaji Sylvain Orè mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu (African court on Human and peoples’ Rights) Mhe. Jaji Sylvain Orè mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 27 Mei, 2021. (PICHA ZOTE NA IKULU).

Kwa upande wake, Mhe. Ore amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa ushirikiano ambao Mahakama hiyo imeupata kwa kipindi chote cha uongozi wake, na amemhakikishia kuwa Tanzania ni sehemu sahihi ya Mahakama hiyo kuwepo kutokana na uwepo wa amani, utulivu na mandhari ya kuvutia.

Mhe. Ore ambaye ametumia fursa hiyo kumuaga Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa katika kipindi cha uongozi wake Mahakama imeendelea kutekeleza majukumu yake vizuri katika kufikia matarajio ya Bara la Afrika na kwamba amefurahi kupata nafasi ya kumueleza Mhe. Rais Samia kuhusu Mahakama hiyo.Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news