Sekta binafsi yakiri matokeo chanya kupitia Rais Samia

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) amesema sekta binafsi imeanza kuona matokeo ya juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, ambapo kufuatia ziara yake nchini Kenya, sekta binafsi ya Kenya na ya Tanzania wamekubaliana kuanzisha soko la pamoja la bidhaa ambalo litawawezesha wafanyabiashara wa pande zote kuuza na kununua bidhaa sokoni hapo na pia mpango wa bajeti ya mwaka 2021/22 umezingatia maoni ya sekta binafsi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Kikao na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa TPSF, Angelina Ngalula wakati Rais Samia alipokutana na viongozi wa TPSF katika mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, viongozi hao wameomba Serikali kuendelea kutilia mkazo juhudi za kuboresha zaidi mazingira ya kufanya biashara (Blue Print), kusimamia ulipaji wa kodi, kusimamia manufaa ya ndani (local content) katika miradi mikubwa, kufanya utafiti, kuvutia mitaji, uwekezaji katika maeneo ya kimkakati na kutilia mkazo kuendeleza kilimo ambacho kinaajiri Watanzania wengi.

Viongozi hao wamemuahidi Rais Samia kuwa wapo tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha wanakuza zaidi uzalishaji kupitia sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wa nchi, kuzalisha ajira na kuinua ustawi wa jamii. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi mbalimbali (Wanawake) wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya kumbukumbu na viongozi mbalimbali (Wanaume) wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation) mara baada ya Kikao chao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU).

Kwa upande wake Rais Samia amewapongeza viongozi hao kwa juhudi kubwa zinazofanywa na TPSF kuitikia wito wake wa kutekeleza jukumu la kukuza uchumi na amewahakikishia kuwa Serikali itawaunga mkono katika juhudi zao za kukuza bishara.

Rais Samia ameahidi kufanyia kazi maoni yao pamoja na maoni mengine yatakayotolewa katika mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) unaotarajiwa kufanyika Juni, 2021.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news