Serikali yawaagiza maafisa Afya kuwafanyia abiria vipimo vya Corona Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere

Na Mwandishi WAMJW, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi amewataka maafisa Afya katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na makampuni ya kifedha yanayotoa huduma za kupokea malipo kwa Abiria wanaowasili nchini na kufanyiwa vipimo vya Covid 19, kufanya kazi kwa ushirikiano na ufanisi, ili kuweza kutoa huduma yenye ubora na kutowachelewesha Abiria wanaopatiwa huduma katika Uwanja huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi akizungumza na watumishi wa wizara hiyo ambao ni maafisa afya wanaohudumu katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na wadau wanaotoa huduma za kifedha kwa abiria wanaofanya malipo ya kipimo cha Covid 19 wanapowasili nchini, ili kujua changamoto zinazojitokeza katika utoaji wa huduma hizo na maboresho ambayo yamefanyika ili kuhakikisha huduma hizo zinatolewa kwa wakati.

Prof Makubi amesema hayo katika ziara yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,yenye lengo la kukagua huduma za upimaji wa Covid 19 kwa abiria wa wanaowasili nchini zinazotolewa na maafisa Afya wa uwanja huo na kuangalia changamoto zinazopelekea kuwepo kwa ucheleweshaji wa huduma kwa abiria hao kama zimefanyiwa kazi.

Katibu Mkuu amesema kitendo cha kuchelewesha kutoa baadhi ya huduma kwa baadhi ya abiria wanaowasili nchini kamwe hakivumiliki, hivyo watendaji wanaohusika wajaribu kuondoa vikwazo vinasababisha kuchelewesha huduma hizo, ambazo zimekuwa kero kwa baadhi ya abiria wanaowasili nchini na kutakiwa kufanyiwa vipimo vya Covid 19 uwanjani hapo.
Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Aifello Sichwale akizungumza na maafisa afya wanaohudumu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa ziara ya Katibu mkuu wizara ya Afya, ambapo amewataka kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wengine ili kuweza kutoa huduma bora za upimaji wa Covidi 19 kwa abiria wanaowasili nchini kupitia uwanja huo wa ndege.
Maafisa Afya wanaotoa huduma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na wadau kutoka makampuni yanayotoa huduma za kifedha katika Uwanja huo, wakimsilikiza Katibu Mkuu wizara ya Afya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Prof Abel Makubi (hayupo pichani) mara baada ya kufanya ziara uwanjani hapo kukagua namna huduma za upimaji wa Covid 19 zinavyofanyika kwa abiria wanaowasili nchini.

“Kweli kuna ucheleweshaji unaoweza kufanyika na mtu akakuvumilia wala asikereke lakini ikishafika masaa mawili hiyo haikubaliki, hebu tuondoe hivi vikwazo vinavyosababisha huduma kuchelewa ili wananchi waweze kupata huduma na tusionekane kero kwao,"amesema Prof Makubi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichwale amemuondoa hofu katibu Mkuu katika kusimamia huduma zinazotolewa katika Uwanja huo, ambapo amesema atahakikisha anasimamia maafisa Afya uwanjani hapo na kuhakikisha wanatoa huduma sahihi na watashirikiana na wadau wengi katika kuhakikisha wageni wanaoingia nchini wanapata huduma zenye kiwango cha ubora wa hali ya juu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news