Maelfu ya mizoga ya samaki imebainika katika mwambao wa ziwa nchini
Lebanon ambapo mamlaka nchini humo zinaendelea na jitihada za kupata
ukweli kufahamu kiini cha tatizo hilo, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI
(Mashirika).
Wafanyakazi nchini humo wamekusanya zaidi ya tani
40 ya mizoga ya samaki hao kwa siku mbili huku maelfu ya samaki
yakishuhudiwa yakiendelea kuelea katika mwambao katika eneo la Ziwa
Qaraoun.
Picha ya juu ikionyesha mizoga ya samaki waliokutwa mwambao mwa ziwa eneo la al-Oaraoun Magharibi mwa Wilaya ya Begaa iliyopo Mashariki mwa Lebanon Aprili 29, 2021/ An aerial picture shows dead carp fish flushed to the shores of al-Qaraoun reservoir in Lebanon's Western Beqaa District in the country's east on April 29. (Photo by AFP via Getty Images).
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ufaransa (Agence France-Presse) wafanyakazi wengi wa umma wameendelea kutumia matoroli na vifaa vingine vya ujenzi kwa ajili ya kuzoa samaki hao.
Mizoga ya samaki ikionekana katika mwambao wa Ziwa Oaraoun nchini Lebanon/ Dead (Photo by AFP via Getty Images).
Ziwa Qaraoun mbalo lilijengwa kwa ajili ya kusaidia kuepusha madhara katika Mto Litani Mashariki mwa Lebanon limechafuliwa zaidi kutokana na shughuli za binadamu.
Hatua ambayo inaelezwa huenda, vifo hivyo kama si sumu basi samaki hao wamekufa kutokana na virusi ambavyo bado uchunguzi haujaweka wazi majibu kulingana na AFP.
Wavuvi mjini humo wamesema kuwa, vifo hivyo vya samaki ni tishio kubwa na hawajawahi kulishuhudia katika maisha yao tangu kuundwa kwa bwawa ambalo lilikuja kuzaa Ziwa Qaraoun mwaka 1959.
Ziwa hilo lipo Magharibi mwa wilaya ya Begaa Mashariki mwa Lebanon/ The lake sits in the Western Beqaa District in east Lebanon. (Photo by AFP via Getty Images).
Kwa mujibu wa ripoti za karibuni zinaeleza kuwa Ziwa Qaraoun lilifungwa na Serikali ya Lebanon mwaka 2018 baada ya uchafuzi mkubwa wa mazingira yake, hivyo kuonekana samaki hawafai kuliwa kwa usalama wa bianadamu.
Tags
Kimataifa