Na Diramakini (diramakini@gmail.com)
Timu
ya wataalamu kutoka Tanzania imekutana na timu ya wataalamu kutoka
Kenya Jijini Arusha kujadili njia za kuondoa vikwazo visivyo vya
kibiasha baina ya Nchi hizo kwani vimekuwa vikiathiri biashara, mkutano
wa leo Mei 26, 2021 ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Biashara wa
pande zote mbili utakaofanyika tarehe 29 Mei 2021.
Mwenyekiti
wa timu ya majadiliano ambae ni Mkurugenzi wa Mtangamano wa Biashara
kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara – Tanzania, Bw. Ally Gugu akiongea
na washiriki (hawapo pichani) wakati wataalamu hao walipokutana leo
Jijini Arusha kujadili njia za kuondoa vikwazo visivyo vya kibiasha
baina ya Tanzania na Kenya. Kulia ni mwenyekiti mwenza kutoka Kenya
ambae ni Mkuu Kitengo cha Biashara baina ya Nchi na Nchi, Idara ya
Biashara na Maendeleo ya Ujasiriamali Bw. Michael Mandu.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifutilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifutilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.
Mkutano
huu utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 28 Mei
2021 na baadaye mkutano wa Mawaziri tarehe 29 Mei 2021. Mkutano huo
utahitimishwa kwa mawaziri wa Kenya na Tanzania kufanya ziara katika
mpaka wa Namanga tarehe 30 Mei, 2021 kujionea shughuli za biashara
zinavyofanyika katika mpaka huo.
Ujumbe
wa Tanzania katika timu wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Mtangamano
wa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu wakati
ujumbe wa Kenya umeongozwa na Bw. Michael Mandu, Mkuu wa Biashara baina
ya Nchi na Nchi, Idara ya Maendeleo ya Biashara na Ujasiriamali.
Mkutano
wa wataalamu umetoa fursa ya kujadili masuala yote yanayokwamisha
biashara baina ya pande zote mbili ambapo masuala yaliyowasilishwa na
Kenya kujadiliwa ni pamoja na kutotoa upendeleo kwa sigara, maziwa,
bidhaa za nyama, kutoka Kenya, tozo ya kuingia kwa wafanyabiashara
(business pass) kufanya kazi za muda mfupi za kitaalamu.
Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukifutilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.
Timu ya wataalam kutoka Tanzania na Kenya wakifuatilia mkutano wa madajiliano ya kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.
Kwa
upande wa Kenya, baadhi ya masuala ambayo Tanzania imewasilisha
kujadiliwa ni kuongezwa bei ya vinywaji baridi (uplifting) kutoka
Tanzania, kutoza ushuru wa forodha bidhaa za glass, kuzuia mahindi
kutoka Tanzania, bei kubwa ya ushuru wa stempu katika bia, kubadili
mfumo wa uingizaji mizigo mikubwa ambapo gharama za uingizaji mizigo
Kenya zimeongezeka na kuathiri biashara.
Katika
kutekeleza maagizo ya Wakuu wa nchi (Tanzania na Kenya) mawaziri wa
seka husika kutoka watakutana na kujadili juu ya vikwazo hivyo katika
mkutano wao utakaofanyika tarehe 29 Mei, 2021 jijini Arusha.
Tarehe
4 – 5 Mei, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Samia Suluhu Hassan alifanya ziara rasmi nchini Kenya ambapo katika
ziara hiyo Mhe. Samia Hassan Suluhu na Mwenyeji wake Mhe. Uhuru Kenyatta
pamoja na mambo mengine, walielekeza Mawaziri wa Biashara wa pande zote
wakutane na kujadili vikwazo vya kibiashara ambavyo vinaathiri biashara
kwa lengo la kuviondoa.
Tags
Kimataifa