Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Aboubakar Kunenge ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sikukuu ya mkulima iliyofanyika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo TARI Kibaha tarehe 28/5/2021 akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uhaulishaji wa Teknolojia na Mahusiano wa TARI, Dkt. Mwakasendo juu ya majukumu ya idara ya uhaulishaji wa teknolojia na mahusiano.
Mkurugenzi alisema, idara inahaulisha
teknolojia za uzalishaji wa zao la miwa na mazao ya mizizi kwa wakulima kwa kutumia mbinu mbalimbali kama vile shamba darasa, shamba la mfano, njia ya utangazaji kupitia vyombo vya habari, meseji kupitia simu ya mkononi, vipeperushi vilivyoandaliwa kwa lugha nyepesi.
Pia Dkt. Mwakasendo alimwambia Mgeni rasmi kuwa njia nyingine ni kutumia maonyesho ya sikukuu ya wakulima, maonesho ya Nanenane na kupitia mashamba mahiri yaliyopo kwenye viwanja vya Nanenane.
Idara pia ina jukumu la kuhamasisha kilimo bora cha miwa na mazao ya mizizi kwa wakulima ili kuwawezesha kuzalisha kwa tija na hivyo kuongeza kipato, uhakika wa chakula, lishe bora na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini. (Picha na TARI).
Tags
Picha