TASAC yafuta tozo saba zilizokuwa kero, yawezesha unafuu bandarini

Na Diramakini (diramakini@gmail.com)

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) katika kipindi cha miaka minne limefanikiwa kufuta tozo saba nyanyaso zilizokuwa ni kero kwa wadau katika sekta ya maji, hivyo kuleta unafuu wa utoaji wa mizigo bandarini.
Mafanikio hayo ya TASAC yametangazwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Uhusiano wa TASAC, Nicholous Kinyariri wakati akiwasilisha mada ya Ifahamu TASAC katika warsha ya Wahariri na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Habari.

Mbali na hilo, amesema TASAC imefanikiwa pia kudhibiti nyaraka za mizigo na kuisaidia serikali kukusanya Kodi yake ipasavyo kwa mizigo inayotoka nje ya nchi.

Kulingana na Kinyariri, TASAC, pia imefanikiwa kutoa leseni 804 za kampuni za uwakala wa forodha na leseni 20 za uwakala wa Meli.

Pia Kinyariri amesema katika kipindi hicho Cha miaka Minne wamefanikiwa kutoa gawio la zaidi ya shilingi Bilioni-40 kwa serikali.

Kuhusu changamoto zinazowakabili wamesema ni uelewa Mdogo wa wananchi kuhusu majukumu yanayofanywa na TASAC hivyo kuamua kuja na Mpango wa kuwafikia wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari kufikisha ujumbe kwa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news