NA EMMANUEL MBATILO, Dar es Salaam
Kuelekea Siku ya Vipimo Duniani Mei 20,Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewataka watumiaji wa Vipimo katika sekta ya afya nchini kuhakikisha vipimo hivyo vimepitishwa na Shirika hilo kabla havijatumika.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mkumba amesema wamekuwa wakikutana na Changamoto kubwa ya watumiaji wa Vipimo kutokuwa na uwelewa wa kufanya uhakiki wa vifaa vyao ili kuboresha huduma wanazozitoa kwenye sekta za afya.
Afisa vipimo Mwandamizi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Bw.Ramadhan Mfaume akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”.
“Vipimo vinavyotumika katika sekta ya afya ni muhimu vikahakikiwa na kujulikana ubora wao kwa kufanya hivi itakuwa inalinda afya ya wagonjwa kwasababu daktari anaweza kufanya maamuzi kupitia vipimo vinavyotoka maabara vikiwa vipimo sio sahihi vinaweza kupelekea kumpatia madhara mgonjwa”. Amesema Bw.Mfaume.
Aidha Bw.Mfaume amesema kuwa dhumuni la kauli mbiu ya mwaka huu ni kuleta uelewa katika jamii jinsi gani vipimo kwenye sekta ya afya vina umuhimu kama tunavyotambua vipimo katika sekta ya afya vinatumika kugundua, kutambua na kutibu magonjwa.
Mkuu wa Maabara ya Vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam kuelekea Siku ya Vipimo Duniani yenye kauli mbiu “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”. (PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Kwa upande wake Mkuu wa Maabara ya vipimo (TBS), Bw.Joseph Mahila amesema katika maadhimisho ya Siku ya Vipimo kwa mwaka huu watajikita zaidi katika sekta ya afya hasa kutokana na kauli mbiu ya mwaka huu “VIPIMO KATIKA SEKTA YA AFYA”.
Tags
Habari