MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imezifungulia akaunti zote za wafanyabiashara ilizokuwa zimeshikiliwa kutokana na madeni ya kodi
Hayo yamesemwa leo mjini Morogoro na Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa (TRA), Richard Kayombo, wakati akitoa mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jukwaa la Wahariri (TEF).
Kayombo amesema hivi sasa mamlaka hiyo inaingia mikataba ya makubaliano na wafanyabiashara hao wenye madeni ili walipe kwa utaratibu maalum.
Amesema sheria inairuhusuTRA kushikilia akaunti ya mtu yeyote ambaye anadeni la kodi kama njia ya kupata fedha ambazo serikali inadai.
Lakini Kayombo amesema uamuzi wa kushikilia akaunti ya mfanyabiashara huwa ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kama majadiliano kushindikana.
"Sikawaida kushikilia akaunti ya mfanyabiashara na uamuzi huu mara nyingi unakuwaga wa mwisho kabisa baada ya jitihada zingine kushindikana ikiwemo majadiliano na mhusika," amesema Kayombo
"Tumeamua kuziachia hizi akaunti ili sasa tuwe tunakaa mezani na kujadiliana na wafanyabiashara wenye madeni namna bora ya kulipa taratibu taratibu na tunaachana na ule wa kushikilia akaunti zao," amesema Kayombo....(NIPASHE).
Tags
Habari