"Katika robo ya tatu ya Januari- Machi majina ya uhamisho yatatoka April 10 na robo ya mwisho ya Aprili-Juni majina ya uhamisho yatatoka Julai 10,"amesema.
Aidha, Prof.Shemdoe amebainisha kuwa majina ya watumishi wote watakaohamishwa yatawekwa kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ambayo ni www.tamisemi.go.tz.
Pia amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa yote nchini kuwasilisha orodha ya watumishi wa kuhama ofisi ya Rais-TAMISEMI kila tarehe 5 ya mwezi unaofuata baada ya robo mwaka.
Aidha, amewataka Makatibu Tawala wote kutokupitisha maombi ya watumishi wanaotaka kuhamia kwenye majiji, manispaa na miji kwa kuwa maeneo hayo yana idadi kubwa ya watumishi.
Aidha, Profesa Shemdoe amewataka Makatibu Tawala kuwapa kipaumbele watumishi wenye changamoto mbalimbali zilizothibitishwa.
Pia aliwataka watumishi wote kubaki kwenye vituo vyao na barua za uhamisho zitatumwa kwa waajiri wao na wataona majina yao kwenye Tovuti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Pia amewataka watumishi kujihadhari na matapeli wanaotaka fedha kwa ajili ya kufanikisha uhamisho wao kwa kuwa Uhamisho ni bure na ni haki ya kila mtumishi.
Amesema kuwa, Barua za Uhamisho za kipindi cha nyuma ambazo zilishafika Ofisi ya Rasi TAMISEMI zinashughulikiwa na majina yatatolewa kila mwezi mpaka Juni 30 kabla utaratibu mpya haujaanza kutumika.