Mikoa ya Kagera na Mara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku 17/05/2021 umeletwa na mchambuzi Daniel Masunga
Mikoa ya Geita, Mwanza na Simiyu: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kilimanjaro, Arusha , Manyara, Morogoro, pamoja na (Visiwa vya Unguja na Pemba): Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Njombe, Iringa, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora na Katavi, Ruvuma, Kigoma, Shinyanga, Mtwara, pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
KIWANGO CHA JUU ZAIDI CHA JOTO NI NYUZI JOTO 32 ( 32°C ) KATIKA MJI WA TANGA.
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 30 kwa saa; kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa Kiasi.
Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 19/05/2021: Mabadiliko Kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 17/05/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Tags
Habari