Ikiwa zimepita siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutoa msamaha wa wafungwa, tayari wafungwa wawili kutoka gereza la Mkuza lililopo Kibaha wamefariki baada kupigwa na wananchi wenye hasira kali wakati wakijaribu kuiba, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.
Wafungwa hao walipata msamaha huo Aprili 12, mwaka huu wakitokea gereza la Mkuza lililopo Kibaha, lakini hata hivyo baada ya kutoka waliendeleza tabia ya wizi na hivyo kunasa mikononi mwa wananchi wenye hasira kali.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema kuwa, tukio hilo lilitokea Mei 8, mwaka huu saa 12 alfajiri huko Kibaha kwa Mathias .
Nyigesa amewataja wafungwa hao wawili kuwa ni Ramadhani Mohamed 28 (Seven) Mndengereko mkazi wa kwa Mathias Kibaga na Idd Hamis(30)Mzaramo mkazi wa Jamaika Kibaha.
Amesema,siku chache baada ya wafungwa hao kusamehewa na Rais kutoka kifungoni katika gereza la Mkuza Kibaha waliendeleza tabia ya wizi katika katika maduka na maeneo mbalimbali lakini waliingia mikononi mwa wananchi na hivyo kupata kipigo.
Amesema kuwa,watu hao baada ya kukamatwa na wananchi hao walipigwa kwa kutumia silaha za Jadi, Mawe,Mapanga na fimbo waliumia vibaya lakini hatahivyo walifia njiani wakati wakiwa wanakimbizwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.
Aidha,kutokana na tukio hilo Kamanda Nyigesa alitoa rai kwa wananchi kuacha kuchukua sheria mkononi na badala yake wawaachie vyombo vya dola kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria .
Tags
Habari