Watahiniwa 90,025 wa Kidato cha Sita kufanya mitihani kesho

Leo Mei 2, 2021 jijini Dar es Salaam, Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema jumla ya watahiniwa 90,025 wa kidato cha sita kwa upande wa Tanzania Bara na Visiwani wanatarajia kuanza mitihani yao Mei 3, mwaka huu hadi Mei 25, mwaka huu.

Pia 6,973 watafanya mitihani ya kozi za ualimu katika ngazi ya stashahada na cheti, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI (Dar es Salaam).
Katibu Mtendaji wa NACTE, Charles E. Msonde amesema, Mitihani hiyo itafanyika katika shule za sekondari 804 huku vituo vya kujitegemea vikiwa 248 na vyuo vya ualimu 75 nchini kote.

Dkt.Msonde amesema kuwa,watahiniwa 90,025 wa kidato cha sita waliosajiliwa kufanya mtihani kati yao watahiniwa wa shule 81,343 na 8,682 ni wakujitegemea.

Amesema, kati ya watahiniwa wa shule 81,343 waliosajiliwa wanaume ni 46,233 sawa na asilimia 56.84 na wanawake ni 35,110 sawa na asilimia 43.16 huku watahiniwa wenye mahitaji maalumu wakiwa 118 kati yao 95 ni wenye uoni hafifu na 23 ni wasioona.

Pia Dkt.Msonde amesema kuwa, watahiniwa wa kujitegemea ni 8,682 huku wanaume 5,759 sawa na asilimia 66.33 na wanawake 2,923 sawa na asilimia 33.67 huku asiyeona akiwa ni mmoja.

Amesema, watahiniwa 6,973 wa ualimu wanaofanya mitihani ya kozi kati yao 2,187 ni ngazi ya stashahada huku 4,786 ni ngazi ya cheti.

Dkt.Msonde amesema kuwa,kati ya watahiniwa 2,187 wa ngazi ya stashahada waliosajiliwa ni 1,446 sawa na asilimia 66.12 ni wanaume na 741 sawa na asilimia 33.88 ni wanawake.

"Kati ya watahiniwa 4,786 wa ngazi ya cheti waliosajiliwa 2,637 sawa na asilimia 55.10 ni wanaume na 2,149 sawa na asilimia 44.90 ni wanawake huku watahiniwa wa ngazi ya cheti wenye uoni hafifu wakiwa 3 na wawili ni wasioona,"amesema.

Dkt.Msonde akizungumzia kuhusiana na maandalizi amesema yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa mitihani husika, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote muhimu zinazohusu mitihani hiyo katika mikoa na halmashauri zote Tanzania Bara na Visiwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news