Na James K. Mwanamyoto-Karema
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewataka viongozi katika Taasisi za Umma kutumia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu kutembelea maeneo ya pembezoni ili kusikiliza na kutatua kero na changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma, ikiwa ni pamoja na kupokea maoni na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha Utumishi wa Umma nchini.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumzia masuala ya kiutumishi na watumishi wa Tarafa ya Karema Wilayani Tanganyika.
Watumishi wa Umma wa Tarafa ya Karema wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu Mkuu huyo ya kuhimiza uwajibikaji na kutatua changamoto za watumishi wa tarafa hiyo.
Mwalimu Baraka Ambonile wa Shule ya Msingi Kapalamsenga, Tarafa ya Karema Wilayani Tanganyika akiwasilisha changamoto yake ya kiutumishi kwa Dkt. Laurean Ndumbaro wakati wa ziara ya kikazi ya Katibu mkuu huyo tarafani humo.Dkt. Ndumbaro amesema hayo katika Tarafa ya Karema akiwa ameambatana na
Katibu Mkuu, Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome pamoja na
Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John
Jingu ambao kwa pamoja wamehimiza uwajibikaji na ufanisi kiutendaji
katika taasisi zinazosimamia utoaji wa haki kwa wananchi.
Aidha
Dkt. Ndumbaro amewata viongozi katika Taasisi za Umma kuhakikisha
wanajenga utamaduni wa watumishi kufanya kazi kwa bidii, na kuongeza
kuwa utamaduni huo utajengwa kwa kutambua na kuwapongeza wanaofanya kazi
kwa juhudi na maarifa na kwa wanaolegalega warekebishwe ili waweze
kufanya kazi kwa ufanisi.
Amefafanua kuwa, watumishi wanaochapa
kazi wakipongezwa kwa kuandikiwa barua au kupewa cheti kutokana na
mchango wao ndio njia pekee itakayowawezesha waajiri kujenga utamaduni
wa watumishi kufanya kazi kwa bidii na weledi. tofauti na kuchukua hatua
hiyo morali ya watumishi wanaowajibika ipasavyo itashuka kwa kiwango
kikubwa.
Akizungumzia kuhusu mtazamo hasi wa baadhi ya watumishi
wa Tarafa ya Karema kuamini kuwa wanafanya kazi katika mazingira magumu
sana, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt.
John Jingu amewataka kubadili fikra zao kwani Serikali imewaajiri kwa
lengo la kuwahudumia wananchi wa eneo hilo na si kuwapa adhabu kama
baadhi yao wanavyodhani.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Mathew Kirama akipokea hoja za masuala ya kiutumishi za watumishi wa Tarafa ya Karema toka kwa Afisa wa tarafa hiyo, Bw. Mbonimpaye Nkoronko kwa lengo la kuzifanyia kazi changamoto hizo.
Dkt. Jingu amewaambia watumishi hao kuwa, Utumishi wa Umma
ni popote hivyo amewataka kutumia fursa zilizopo katika Tarafa ya Karema
kuongeza kipato na kuboresha maisha yao.
Naye, Katibu Mkuu,
Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome amesema katika sheria na
masuala ya katiba ndio taifa linapata mfumo wa utoaji haki ambapo haki
zipo za aina nyingi kama vile haki madai, haki jinai pamoja na haki
utawala inayosimamiwa na Katibu Mkuu - UTUMISHI kuhakikisha inakwenda
sawasawa ili wananchi wapate huduma bora katika Taasisi za Umma.
Sanjali
na hilo, Prof. Mchome amesema, migogoro ya ardhi iliyopo Karema ni
changamoto kama ilivyo kwenye maeneo mengine, hivyo amewataka watumishi
kushirikiana na wananchi hususani wazee wenye busara katika kutatua
migogoro hiyo kwa njia ya usuluhishi badala ya kukimbilia Mahakamani
kwani Mahakama kwa mujibu wa Katiba ni chombo cha mwisho cha utoaji
haki.
Ziara ya Makatibu Wakuu hao mkoani Katavi ililenga
kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi pamoja na kutatua changamoto
zinazowakabili watumishi mkoani humo.
Tags
Habari