Watakiwa kuwapa watumishi wa ndani uhuru wa kuanzisha familia binafsi

Na CATHERINE MBIGILI, Iringa

WAAJIRI wa watumishi wa kazi za ndani wametakiwa kuwapa uhuru wa kuanzisha familia binafsi watumishi wao badala ya kuwazuia kujiingiza katika mahusino licha ya umri kuwaruhusu kufanya hivyo.

Baadhi ya watumishi wa ndani wakiwa katika moja ya semina waliyoandaliwa hivi karibuni. (Picha na Mtandao).

Mwanasaikolojia,Leonard Mgina ameyasema hayo mjini hapa wakati alipozungumza na Diramakini Blog.

Mgina amesema, zipo athari nyingi za kisaikolojia zinazoweza kuwakumba watumishi wa ndani endapo haki zao za faragha zitazuiliwa bila sababu za msingi.

Amesema, waajiri wanapaswa kufahamu kuwa watumishi wa kazi za ndani wana haki za kuwa na mahusiano kwani nao ni binadamu kama binadamu wengine.

"Nimesikia baadhi ya wafanyakazi wanasema waajiri wengi wanawafungia ndani na kuwazuia wasikutane na watu nje ya mazingira yao ya kazi hali inayowafanya kukosa haki zao za msingi ya kukaa faragha na weza wao muda wa kazi unapoisha ili suala hatuwezi kulifumbia macho,"amesema Mgina.

Kwa upande wawaajiri,Regina Kitosi ni mmoja wa waajiri hao yeye anasema wanafanya hivyo ili kuwalinda watumishi hao na magonjwa pamoja na mimba zisizotarajiwa.

Amesema, mara nyingi wazazi wanapokupa binti wa kazi wanatarajia arudi kama alivyokuja sasa linapotokea suala la binti huyo kupata mimba au mtoto wanaolaumiwa ni wao kwamba walimfundisha tabia mbaya.

"Leo hii uchukue mtoto wawatu arudi na mimba unahisi nani atapewa lawama ,hatupendi kuwachunga ila tunatengeneza mazingira ya sisi kutojipotezea uaminifu kwa wazazi waliotuamini na kutukabidhi mtoto,"amesema Regina.

Wakizungumzia saula la kukataliwa kuazisha mahusiano ,Rosemary Mawona ambaye ni mfanyakazi wa ndani yeye anasema zipo changamoto nyingi wanazokumbana nazo katika kazi hiyo ikiwa ni pamoja kudharaulika katika jamii pamoja na kuonekana kama walikotoka wanamaisha magumu jambo ambalo siyo kweli.

Amefafanua kuwa, wafanyakazi wa ndani wanapaswa kuheshimiwa na kuchukuliwa kama wafanyakazi wengine kwani kazi yeyote inayomwingizia mtu kipato ni kazi, haijalishi inafanyika katika mazingira gani.

"Tunahitaji heshima yetu na waajiri wetu watambue kwamba tupo kufanya kazi hatuna maisha magumu tulikotoka ila tumekuja kutafuta tu maisha,"amesema Rosemary.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news