WAZEE MKOANI IRINGA WAMPOKEA MKUU WA MKOA MPYA KWA KISHINDO

Na CATHERINE MBIGILI, Iringa
 
WAZEE Wa Mkoa Wa Iringa wamemkaribisha kwa kishindo Mkuu wa Mkoa mpya,Queen Sendiga huku wakiahidi kumpa ushirikiano endepo atawatumia katika utekelezaji wa majukumu yake.
Hayo waliyazungumza jana wakati wa makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa zamani, Ally Happi, ambaye kateuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora, na Queen Sendiga ambaye kateuliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
 
Omary Nzowa ambaye ni mkuu wa baraza la wazee mkoani hapo, alisema atamkumbuka kiongozi huyo kutokana na utendaji wake wa kazi lakini hana budi kumuaga na kumkalibisha kiongozi mpya na wateendelea kumuombea pamoja na kumpa ushirikiano.
 
Alisema, wao kama wazee wanaujua mkoa wa Iringa vizuri historia yake pamoja na vitongoji vyake vyote hivyo hawata muachia mzigo peke yake katika kuutumikia mkoa wa Iringa.
 
"Sisi wazee tunajivunia sana uwepo wako wote kwa kipindi chote ulichokuwepo Iringa tumeona utendaji wako tunakutakia kila la heri huko uendako ukazidi kuwa kiongozi mwadilifu na unayejali maslahi ya wananchi wako,"alisema Nzowa.
 
Naye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa zamani mkoani hapa, Ally Happi, alisema anaondoka Iringa huku akiwa bado anawapenda wananchi wa mkoa huo kutokana na uchapakazi wao , ushirikiano,pamoja na moyo wa kujitolea waliokuwa nao.
 
Alisema yawezekana aliwakwanza baadhi ya watu kutokana na kusimamia haki katika utendaji wake hivyo kama kuna mtu alimkwanza katika majukumu yake amsamehe.
 
"Naondoka nikiwa bado nawapenda kwa yeyote niliyomkwanza anisamehe nilijitoa kwa ajili ya wana Iringa ila ninaimani na huyu kiongozi nawahakikishia kwamba linaondoka jembe linakuja jembe,"alisema.
 
Alisema, katika uongozi wake alisimamia haki alitatua migogoro alitembelea kila kijiji anasema yote hayo alifanya kwa ajili ya wana Iringa.
 
Hivyo aliwaomba wakazi wa Iringa wasimtenge kiongozi wao mpya wasirudi nyuma wala kumkatisha tamaa bali waoneshe ushirikiano katika ngazi zote.
 
"Nikuahidi Kiongozi wakazi wa Iringa ni wachapakazi,wanajituma,wana moyo wa kujitolea wanalima wanachangia miradi wakikupenda wamekupenda hawana moyo wa unafiki,"alisema Happi.
 
Naye mkuu mpya wa Mkoa alisema, hajaja kufanya kazi kama kiongozi amekuja kufanya kazi na wananchi wa Iringa ili kuendeleza mambo yote kiuchumi na kukaa na kamati zote pamoja na wafanyabiashara.
 
Pia aliahidi kusimamia haki na kushughulikia changamoto zote za wana Iringa ikiwa ni pamoja na kusimamia llani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo amekabidhiwa na uongozi wa chama.
 
"Naahidi kufanya kazi na ilani ya chama ambayo nimekabidhiwa leo asubuhi na uongozi wa chama ili kutekeleza yale yaliyoelekezwa ndani ya Ilani katika kuleta maendeleo,"alisema.
 
Pia alisema atasimamia na kuendeleza kaulimbiu ya 'Iringa Mpya' ambayo iliazishwa na kiongozi wa zamani huku akichanganya na yake inayosema uwajibikaji rafiki wa maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news