Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndungulile amesema kuwa wizara yake itahakikisha inaimarisha mitandao ya simu hadi vijijini ili kuwawezesha wakulima kupata habari za kutosha na elimu za mazao mbalimbali zinazotolewa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).
Waziri Ndungulile ameyasema hayo wakati akizungumza na watafiti wa kilimo pamoja na watumishi wa taasisi hiyo leo Mei 10,2021 katika viwanja wa Jamhuri yanapoendelea maonesho ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambapo taasisi inashiriki kuonesha namna teknolojia inavyotumika kuchochea mapinduzi ya kilimo nchini.
Dkt. Ndungulile amesema wizara yake inatambua mchango mkubwa unaotolewa na watafiti wa kilimo katika kuwasaidia wakulima ambapo amesema watahakikisha wanaboresha teknolojia katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wakulima kupata habari za kiutafiti kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii. (Picha zote na Junior Mwemezi -Idara ya Habari na Mawasiliono TARI makao makuu).
Tags
Habari