Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea msaada wa Vifaa mbalimbali
vya michezo pamoja na fulana vitakavyotumika katika Maadhimisho ya Wiki
ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika
Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 ambayo
yatashirikisha Taasisi za Serikali na binafsi.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi, wakionesha mfano wa fulana mojawapo kati ya mia nne (400) zilizokabidhiwa na NMB zitakazotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Vifaa hivyo ni pamoja na mipira kumi (10) kwa ajili ya michezo
mbalimbali, fulana mia nne (400) na Vikombe vitatu (3) vitakavyogawiwa
kwa washindi wakati wa Maadhimisho hayo, vilikabidhiwa na Meneja wa
Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi kwa Kamishna wa Utawala na Fedha
wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza kwa niaba ya Kamishna
Jenerali wa Jeshi hilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Vifaa
hivyo leo jijini Dodoma, bwana Mlozi amesema NMB inatambua mchango wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kuokoa Maisha na Mali za Watanzania,
msaada huu utakuwa chachu katika kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya
Zimamoto na Uokoaji Kitaifa inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (Wapili kulia) akimkabidhi baadhi ya Vifaa vya michezo Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza (Wapili kushoto), vilivyotolewa na NMB vitakavyotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Bwana Mlozi amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia kwa
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo Mbaraka Semwanza kwa niaba ya
Kamishna Jenerali kwa huduma wanazozitoa kwa jamii na kuhakikisha
Maisha na mali za Watanzania vinakuwa salama na kuahidi kuendelea
kushirikiana kwa dhati.
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo,
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka
Semwanza ameshukuru kwa msaada na kusema kuwa utaongeza chachu katika
kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa
yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia
tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021.
Sehemu ya Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza (Wapili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (Wapili kulia) na baadhi ya Maofisa wa Benki ya NMB pamoja na wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya zoezi la kukabidhiwa Vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na fulana zitakazotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. (Picha Zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
“Tunawashukuru sana NMB, benki hii imekuwa mshirika wetu mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, msaada huu tutautumia vyema katika kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa iliyopo mbele yetu inayotarajia kuanza hivi karibuni” Alisema Kamishna Semwanza.
Aidha Kamishna Semwanza ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya zake na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Tumbako ambako Maadhimisho hayo yatafanyika yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”.
Tags
Michezo