Azam FC, Mbeya City zang'ara mitanange ya Ligi Kuu Tanzania Bara

Azam FC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Gwambina FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, anaripoti GODFREY NNKO (Diramakini Blog).

Mtanange huo umepigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Kata ya Chamazi mkoani Dar es Salaam.

Ushindi wa Azam FC umetokana na mabao ya mshambuliaji Mkongo, Mpiana Monzinzi dakika ya 32 na 57.

Sambamba na kiungo Mzawa, Iddi Suleiman (Nado) dakika ya 55 na 74 huku Gwambina FC wakipata bao kupitia Baraka Mtuwi dakika ya 38.

Kwa sasa Azam FC imefikisha alama 63 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa alama moja na Yanga SC ambao pia wana mechi moja mkononi.

Awali Mbeya City imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ndani ya dimba la Sokoine jijini Mbeya.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 18 na George Sangija dakika ya 78.

Kwa matokeo hayo, Mbeya City inafikisha alama 37 baada ya kucheza mechi 31 na kusogea nafasi ya 11.

Wakati Mbeya City wakiwa eneo zuri, wao Coastal Union wanabaki nafasi ya wakiwa alama 33 za mechi 30, kwa mwelekeo huo kuna viashria vya timu hiyo kushuka daraja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news