Benki ya Dunia, Afrika waazimia upatikanaji wa chanjo ya Corona

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Benki ya Dunia imetangaza ushirikiano mpya na Umoja wa Afrika (AU) ili kufadhili upatikanaji na usambazaji wa chanjo za virusi vya Corona (Covid-19) kwa takribani watu milioni 400 barani Afrika.

Mkuu wa Operesheni wa Benki ya Dunia, Axel van Trotsenburg kupitia mkutano wa kimtandao wa Zoom amesema kuwa, benki yake itatoa dola bilioni 12 ili kuhakikisha dozi milioni 400 za chanjo aina ya Johnson & Johnson zitapatikana.
Mtaalam wa afaya akiwa ameshikilia dozi ya chanjo ya Johnson & Johnson katika Hospitali ya Klerksdorp Hospital Februari 18, 2021. (Picha na PHILL MAGAKOE/AFP via Getty Images).

Hiyo ikiwa ni hatua ya kuimarisha mpango wa kupata chanjo kwa Afrika, unaojulikana kama Africa Vaccine Acquisition Task Team (AVATT).

Tangazo hilo lilikuja siku chache baada ya mawaziri wa fedha wa Afrika kufanya kikao na maafisa wa Benki ya Dunia ili kuthamini nanma na kuharakisha upelekaji wa chanjo kwa mataifa ya kiafrika ili kuzuia wimbi la tatu la maambukizi ya Covid-19.

Mradi huo unasemekana kuwa hatua kubwa katika kusaidia AU, kufikia lengo lake la kutoa asilimia 60 ya chanjo kwa watu wa Afrika kufikia 2022.

Katika hatua nyingine, wanaharakati barani Afrika wamesema, hatua ya nchi tajiri kuhodhi chanjo ya COVID-19 kinakwamisha maendeleo ya kuzuia kuenea kwa virusi hivyo barani Afrika.

Mkurugenzi wa Mfuko wa Huduma ya Afya ya UKIMWI (AHF) nchini Kenya, Samuel Kinyanjui amesema, kuhodhi chanjo kunaongeza uhaba wa kitu kinachoweza kuokoa maisha barani Afrika ambako maambukizi mapya yanayoongezeka yanatishia mifumo ya afya ya umma barani humo.

Ametoa wito kwa nchi tajiri kusambaza chanjo zinazozidi mahitaji yao, kuondoa hakimiliki na kuunga mkono kuanzishwa kwa viwanda vya kutengeneza chanjo hiyo barani Afrika.

Mwenyekiti wa Kikanda wa Mtandao wa Taifa wa Watu Waishio na UKIMWI nchini Zimbabwe, Moreni Masanzu amesema, utaifa wa chanjo ni kikwazo kikubwa katika juhudi za Afrika kupambana na janga hilo.

Ameongeza kuwa, upatikanaji wa chanjo ulio na usawa utanufaisha nchi tajiri na maskini, kwani inaweza kuzuia mabadiliko ya virusi vyenye uwezo mkubwa wa kuambukiza na kurudisha hali ya kawaida katika maisha yetu haraka iwezekanavyo.

Hivi karibuni Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa Afrika (Africa CDC) kilitangaza kuwa, hadi sasa nchi za Afrika zimepata dozi milioni 55 za chanjo za COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na shirika la habari la Xinhua, ni asilimia 0.6 ya watu wa bara la Afrika pekee ndio waliopata chanjo kamili ya COVID-19. Morocco, Misri, Nigeria, Ethiopia na Afrika Kusini wanaongoza kwa kupatiwa dozi nyingi za chanjo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news