Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepokea jumla ya dola za kimarekani Bilioni 1.017 sawa na shilingi za kitanzania Trioni 2.3391 kutoka Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia (WB) ambazo ni mkopo wa masharti nafuu, ANARIPOTI DOREEN ALOYCE (Diramakini Blog).
Akiongea na waandishi wa habari leo Juni 6, 2021 Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa, Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia iliidhinisha mikopo mitatu ya masharti nafuu yenye jumla ya dola za Kimarekani milioni 875 sawa na shilingi Trilioni 2.0125 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji miradi ya maendeleo nchini.
"Tarehe 3 Juni 2021 bodi hiyo iliidjinisha mkopo mwingine wenye thamani ya dola za Marekani milioni 142 Sawa na shilingi bilioni 326.6 na kufanya jumla ya mikopo yenye mashariti nafuu iliyoidhinishwa na bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia minne ikiwa na thamani ya dola za Marekani bilioni 1.017 sawa na sh.2.3391.
"Miradi iliyopata idhini ya bodi ni Mradi wa ROADS TO INCLUSION AND SOCIOECONOMIC OPPORTUNITIES PROGRAM (RISE),wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 300,mradi wa Higher Education for Economic Transformation Project (HEET) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 425,mradi wa Digital Tanzania Project (DTP) wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 250 na mradi wa Zanzibar Energy Sector Transformation and Access Project wenye mkopo wa dola za kimarekani milioni 142,"ameeleza Dkt.Mwigulu.
Dkt.Mwigulu ameitaja miradi mingini kuwa ni mradi wa RISE ambao utasaidia kuboresha barabara za vijijini na kutoa fursa za ajira takribani ajira 35,000 kwa wananchi waliopo katika vijiji nufaika pamoja na kujenga uwezo wa usimamizi endelevu wa Barbara za vijijini kwa kuhusisha njia shirikishi za jamii.
"Mradi huu utahusisha ujenzi wa jumla ya kilometa 535 kwa kiwango cha lami katika wilaya sita za mikoa ya Iringa,Lindi,Geita,na Tanga na ukarabati wa maeneo korofi ya barabara za vijijini nchi mzima,"amesema Dkt Mwigulu.
"Kuna mradi wa DTP utasaidi kuongeza upatikanaji wa huduma bora za mtandao wa Inaneti na kuboresha huduma za Umma kwa kutumia digitali kwa kustawisha ekologia ya kidigitali nchini,kuhakikisha uunganishaji wa kidigitali kwa watanzania wote na kuboresha jukwaa la huduma za kidigitali.
"Mradi wa ZESTA utasaidia kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora nanza uhakika za umeme visiwani Zanzibar ikiwa ni pamoja nankujenga mitambo ya nguvu ya jua na msongo wa kV 132 wa kusafirishia umeme katika visiwa hivyo.
"Vile vile mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 150 kwa ajili ya mradi wa Boosting Inclusive Growth for Zanzibar (BIG-Z),unategemewa kuwasilishwa katika katika vikao vya bodi ya Benki hiyo tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kupata idhini,mradi huu utasaidia kuboresha miundombinu ya mijini katika miji ya Unguja na Pemba kwa kujenga na kuboresha barabara za lami ,mifumo ya maji taka ,mifereji ya maji ya mafuriko ,maeneo ya uthibiti mjini Unguja na Pemba ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na uwekezaji na kukuza utalii katika visiwa vya Zanzibar,"amefafanua Dkt.Mwigulu.
Kuhusu deni la taifa amesema, deni la taifa,likijumuisha la sekta binafsi hadi mwisho wa Aprili 2021 ni dola za Marekani milioni 31,986.7 kati ya deni hilo deni la nje ni dola za Kimarekani milioni 24,477.6 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1.
"Deni la serikali ni dola za Marekani milioni 26,416.8 sawa na bilioni 60,719.01 ikijumuisha deni la nje ni dola za Marekani Milioni 18,907.7 na deni la ndani ni dola za Marekani milioni 7,509.1 sawa na shilingi bilioni 17,259.9,"ameeleza Dkt.Mwigulu.
Hata hivyo, amesema kuwa deni hili ni imilivu na bado nchi ipo katika hatua nzuri ya kiuchumi.
Tags
Habari