BOSI WA TANRODAS MHANDISI MFUGALE AFARIKI

NA MWANDISHI DIRAMAKINI
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini  Tanzania (TANROADS), Mhandisi Patrick Aron Mfugale amefariki dunia leo Juni 29, 2021.

Kwa mujibu wa taarifa za awali ambazo zimeifikia DIRAMAKINI Blog, kifo hicho kimetokea katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
 
"Ni kweli, ila ninaamini taarifa zaidi zitatolewa baadae, vuta subira, inaonekana mzee alizidiwa ghafla akiwa katika kikao,"kimedokeza chanzo hicho.
 
Mzee Mfugale ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Ifunda mkoani Iringa  amehudumu Serikalini kwa miaka mingi tangu mwaka 1977 huku kazi zake zikionyesha matokeo makubwa.
 
Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Consalata Fathers Primary School mjini
Iringa; Mwaka 1975 alihitimu elimu yake ya shule ya upili katika shule ya upili ya Moshi mwaka 1983, alitunukiwa Shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Rocky nchini India.

Mwaka 1991, Mfugale alisajiliwa kama Mhandisi mtaalam na baadaye mwaka 1992, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa barabara za mikoa nchini.

Aidha, mwaka 1994-1995, Mfugale alitunukiwa Shahada yake ya pili katika Chuo kikuu cha Loughborough, Braunshweig nchini Uingereza.

Mwaka 2003 alipokea tuzo ya Distinguished Engineering Accomplishment na kuteuliwa kuwa Mhandisi Mkuu wa madaraja hapa nchini.

Akiwa masomoni nchini Uingereza mwaka 1995, alitafiti na kutengeneza mfumo wa madaraja nchini na mfumo wa usimamizi wa madaraja kwa jina Tanzania Bridge Management System.

Mwaka 2014 alisajiliwa kuwa mhandisi mshauri na kuwa mwanachama wa Chama cha Wahandisi Tanzania.

Ametumia muda wake mwingi kama mtaalamu wa madaraja, ambapo alibuni daraja la Malagarasi lenye urefu wa mita 178 na kujengwa kwa sh.milioni 300.

Miongoni mwa madaraja ambayo aliyasimamia kwa ufanisi wakati wa uhai wake ni pamoja na Daraja la Mkapa huko Rufiji, Daraja la Umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji,Daraja la Rusumo,Daraja la Kikwete huko Malagarasi na Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni.

Mfugale ambaye hadi umauti unamkuta alikuwa mtendaji mkuu wa TANROADS, amesaidia kufanikisha ujenzi wa madaraja 1,400 hapa nchini.

Pia amebuni na kusimamia barabara za kitaifa zenye urefu wa takribani kilomita 36, 258 na alikuwa Mwenyekiti wa kikosi cha ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), inayoendelea kujengwa nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news