NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya, imemuachia huru mwanaharakati wa demokrasia na mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mdude Nyangali baada ya kutompata na hatia katika kesi ya madawa ya kulevya iliyokuwa ikimkabili.
Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer amesema leo Juni 28,2021 kuwa, upande wa Jamhuri ulishindwa kutoa ushahidi wa kutosha kumtia Mdude hatiani.
Awali Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya iliahirisha kusoma hukumu ya kesi ya kada huyo iliyokuwa itolewe Juni 14, 2021.
Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer siku hiyo alisema ameiahirisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake na kubainisha kuwa hukumu hiyo itasomwa Juni 28, 2021.
Mdude alikuwa anakabiliwa na shtaka la kusafirisha heroin gramu 23.4 mwaka 2020.
Tags
Habari