Taarifa zilizoifikia Diramakini Blog muda huu zinaeleza kuwa, Profea Mwesiga Baregu ambaye amekuwa na umaarufu wa aina yake katika medani za siasa za upinzani kwa muda mrefu sasa nchini Tanzania amefariki.
Baregu atakumbukwa kwa kuendesha siasa za kisayansi ambazo si za mikikimikiki ya majukwaani huku akiwa na kauli zenye upeo mpana kwa kumfanya kila mmoja aweze kutafakari.
Wakati wa uhai wake Profesa Baregu licha ya kuwa mhadhiri wa vyuo vikuu mbalimbali nchini pia alitumikia nafasi ya Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema na mlezi wa vijana wa chama hicho.
"Msiba wa Prof. Mwesiga Baregu ni mzito sana. Hakika mchango wake mkubwa katika ujenzi wa demokrasia ya Nchi yetu na haswa katika mchakato wa Katiba ambayo yeye alikuwa Mjumbe wa Tume ya Katiba utakumbukwa Daima. Alikuwa Mwanazuoni wa Umma na Mhadhiri mahiri,"ameeleza Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kutokana na kifo cha Profesa Mwesiga Baregu;
Tags
Habari