Chongolo:CCM haikuabaliani na wanachama wa namna hii

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitawapa nafasi wanachama watakaotaka kuwania uongozi katika chaguzi zote hususani wale ambao hawatahudhuria vikao vya mashina wanayotoka, anaripoti SAID NGUYA. Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo ameyasema hayo katika mkutano wake na wanachama wa chama hicho Kata ya Magila tawi la Geleza Shina namba moja wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Amesema, CCM imejizatiti katika kuimarisha chama hicho katika ngazi ya shina lengo likiwa ni kumuezi muasisi wa chama Rais wa Kwanza wa Tanzania na mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Natoa maelekezo viongozi wote mliotokana na CCM muhakikishe mnashiriki vikao katika mashina mnayotoka, na nataka niseme wakati wa uchaguzi tutaangalia umeshiriki vikao vingapi kama hujawahi kushiki basi wewe sio mwenzetu tutakuengua,”amesisitiza Katibu Mkuu huyo.
Ameongeza kuwa,“Niwasisitize mwakani kuna uchaguzi mkuu wa chama, tutashusha maelekezo, yeyote anayegombea atuletee ushahidi wa minutes za vikao vinavyoonesha alikuwa anashiriki vikao vya mashina, kama unafikiria kugombea nafasi moja ya kigezo utakuwa ushahidi wa muhtasari wa mkutano wa shina,”amesema Chongolo.

Aidha, amewaeleza wenyeviti wa mashina kutowaingiza kwenye muhtasari wanachama waliokuwa hawashiriki vikao kwa sababu hawahudhurii kwenye vikao hivyo kwa sababu wanaona vikao hivyo ni vidogo, lakini wakati wa uchaguzi ukifika wanataka kugombea uongozi.

“Tunataka kuwapa watu ambao kweli wana mapenzi na chama chetu, wanatii na kuheshimu taratibu za chama chetu wanazifuata na kuzishiriki hao ndio watakuwa viogozi ambao hata wakipewa madaraka wataendeleza mfumo huu ambao kwetu ndio msingi wa uhai wa chama,”amesema.
Aidha, ameagiza viongozi wa Serikali kuhakikisha vijana wanaotumia vyombo vya moto kupata mafunzo ya matumizi ya vyombo hivyo ili kuepusha ajali zinazotokana na watumiji wa vyombo hivyo kukosa ujuzi wa kuvitumia.

“Viongozi tuna wajibu wa kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wenye afya ili waweze kuendesha shuguli za kujikwamua kiuchumi, kwanza wapate mafunzo nasisitiza tuna wajibu wa kulinda raia na mali zao,”amesema Chongolo.

Aidha, ameridhia ombi la Diwani wa Kata ya Magila Gereza, Mwajuma Kitumpa aliyeomba kuruhusiwa kwa vyombo vya usafiri aina ya bajaji na pikpiki kwenye eneo hilo ambalo alisema lina changamoto ya usafiri.
Aidha, Chongolo katika kuridhia uamuzi huo wa kuruhusu vyombo hivyo vya usafiri kutumika katika aneo hilo aliagiza kwamba vijana kwanza wapewe elimu ya ujuzi wa kutumia vyombo hivyo ili kuepuka ajali.

Chongolo alikuwa mkoani Tanga katika mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea wanachama na kusikiliza changamoto na kero ngazi za mashina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news