Mkuu wa Gereza Kuu Ukonga mkoani Dar es Salaam, SSP Hamis Lissu akimueleza jambo Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Bw. Sylvester juu ya hali ilivyo katika gereza hilo hivi karibuni. Ni baada ya DPP Mwakitalu kuamua kukiacha kiyoyozi ofisini na kuamua kufanya ziara ya mguu kwa mguu, kuzungumza ana kwa ana na mamlaka, watu au idara zinazoguswa na ofisi yake ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa haki, usawa na kwa wakati.Zinazohusiana,Uamuzi wa DPP wawanasua Wachina sita Kisutu, watimua mbio Hatua hii, ndiyo inayowafanya wananchi wengi wa Jiji la Ilala mkoani Dar es Salaam katika mahojiano maalum na DIRAMAKINI Blog kutaka, kiongozi huyo aombewe na Watanzania wote ili Mungu amuepushe na hila mbaya za muovu shetani, kwani kazi anazofanya zimewapa faraja. Wameyasema hayo muda mfupi,baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Ilala kumfutia mashtaka na kumwachia huru mfanyabiashara Marijan Msofe (53) maarufu Papa Msofe na wenzake wanne. Hatua hiyo inatokana na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu kuwasilisha hati mahakamani hapo akieleza kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.Unaweza kusoma, Ziara ya DPP Mwakitalu, wasaidizi wake magerezani yatoa mwanga kwa wafungwa Msofe na wenzake walikuwa wanakabiliwa wa mashtaka matano likiwemo la kujipatia Shilingi milioni 943 kwa njia ya udanganyifu. Mbali na Papa Msofe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 124/2019 ni Wenceslaus Mtu(49), Mwesigwa Mhingo (36), Josephine Haule (38) na Fadhil Mganga (61). Uamuzi wa kuwafutia kesi hiyo na kuwaachia huru washtakiwa hao umetolewa leo Juni 18, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa. Awali, wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon amedai kuwa DPP ameieleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo. Aidha, baada ya upande mashtaka kueleza hiyo, Shaidi alikubaliana na ombi hilo na kuwafutia mashtaka na kuwaachia huru. Katika kesi hiyo, washtakiwa wanadaiwa kuratibu, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji fedha na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Miongoni mwa mashtaka yao ni kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ambapo washtakiwa hao wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Desemba 2018 na Septemba 2019 jijini Dar es Salaam.Za karibuni, DPP awafutia kesi Mashehe wa Uhamsho na Bosi wa IPTL Harbinder Seth Inadaiwa kuwa wakiwa na nia hiyo walijipatia dola za Marekani 300,000 (Sh 660milioni) kutoka kwa Pasca Camille wakidaiwa kuwa watamuuzia dhahabu yenye uzito wa kilo 200 ambayo wangemsafirishia kwenda Ureno wakati wakijua si kweli. Kwa mara ya kwanza washtakiwa hao walifikishwa Kisutu Desemba 2, 2019 wakikabiliwa na mashtaka hayo. |
Tags
Habari