Freeman Mbowe afunguka mchakato wa kuanzisha Mkoa wa Chato

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mheshimiwa Freeman Mbowe ambaye ni  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema haungani na wanaotaka wilaya ya Chato mkoani Geita ipandishwe hadhi na kuwa mkoa kwa upendeleo.Badala yake, Mheshimiwa Mbowe amesema,Serikali izingatie vigezo vya msingi vya kuipandisha hadhi wilaya hiyo kuwa mkoa.

Ameyabainisha hayo jijini Mwanza alipokuwa katika kikao cha kamati ya utendaji ya chama hicho.

Mheshimiwa Mbowe amesema, uamuzi wa kuifanya Chato kuwa mkoa utakuwa na madhara kwa wakazi wa mikoa ya Geita, Kigoma na Kagera.

Pia, Mheshimiwa Mbowe ametaja madhara yanayoweza kujitokeza kuwa ni baadhi ya wilaya za mikoa ya jirani kumegwa.

Lengo likiwa ni kuunda mkoa huo jambo litakalosababisha matatizo ya huduma za jamii kwa wakazi wa wilaya husika.

Pia Mheshimiwa Mbowe amesema, hatua hiyo itaathiri mila na desturi za wakazi wa wilaya zinazozunguka mkoa huo huku Serikali ikilazimika kutumia fedha nyingi kujenga miundombinu na kuajiri watumishi kwa ajili ya mkoa huo badala ya fedha hizo kuzielekeza katika huduma za jamii.

Amesema, hatua hiyo itazimega wilaya za Biharamulo, Muleba na Ngara ya mkoani Kagera na jimbo la Kakonko la mkoani Kigoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news