Simba SC wameendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Ruvu Shooting 3-0 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
John Raphael Bocco ambaye ni nahodha wa wekundu hao wa Msimbazi amefunga mabao mawili, la kwanza dakika ya 18 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Msumbiji na la tatu dakika ya 88 kwa penalti baada ya kipa wa Ruvu, Abdallah Rashid kumuangusha winga Mghana, Bernard Morrison kwenye boksi.
Morrison, mchezaji wa zamani wa mahasimu, Yanga SC ndiye alimuwekea sawa mshambuliaji Mkongo, Chris Kope Mugalu kufunga bao la pili dakika ya 62.Simba SC imefikisha alama 67 baada ya kucheza mechi 27 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa alama sita zaidi ya Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.
Tags
Michezo