MAMBO SITA ATAKAYOYAFANYA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) TAIFA, SAMIA SULUHU HASSAN KWENYE ZIARA YAKE YA SIKU TATU MKOANI MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi ziara ya siku tatu mkoani Mwanza kuanzia leo Jumapili Juni 13, 2021. Haya ndiyo mambo sita atakayoyafanya;
1. Leo Jumapili Juni 13, 2021 anatembelea na kufungua kiwanda chenye mtambo wa uchenjuaji (kusafisha) wa dhahabu wa shilingi bilioni 13.2 katika eneo la Saba Saba, Ilemela.
2. Leo pia Juni 13, 2021 hiyo hiyo atatembelea na kufungua Jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Kanda ya Ziwa lenye thamani ya bilioni 42 katika Mtaa wa Bolewa, Nyamagana.
3. Kesho Jumatatu Juni 14, 2021 atatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi lenye thamani ya bilioni 699.9 na baadae kuwasalimia wananchi wa eneo la Busisi.
4. Jumatatu hiyo hiyo Juni 14, 2021 atazindua mradi wa maji ulioko wilaya ya Misungwi wa shilingi bilioni 13.2
5. Kesho pia Juni 14, 2021 hiyo hiyo ataweka Jiwe la msingi kwenye mradi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Isaka mpaka Mwanza katika eneo la Fella wenye thamani ya trilioni 3.
6. Juni 15 atahitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano mkubwa kuongea na vijana wa mkoa wa Mwanza kwa niaba ya vijana wote wa Tanzania katika uwanja wa mpira wa Nyamagana.
Tags
Habari