Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar aahidi kutowaangusha ACT-Wazalendo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI Blog

MAKAMU wa Kwanza Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud ameahidi kufanya kazi kwa kujituma ili kufanikisha malengo ya Chama cha ACT-Wazalendo na nchi. 

Makamu huyo alitoa kauli hiyo leo Juni 19/2021 wakati akizungumza kwa mara ya kwanza kama mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kwenye kikao cha kamati kuu cha kawaida kinachofanyika katika Ukumbi wa Lamada Ilala jijini Dar es Salaam.
Pamoja na Masoud pia Kaimu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Dorothy Semu aliwatambulisha wajumbe wapya wa Kamati Kuu ambao ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Wawakilishi Hassan Hamad Omar na Khalifa Mohammed Omar Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.  

Amesema nafasi aliyopewa na chama hicho ya kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imemuheshimisha hivyo atahakikisha anaitendea haki ili kuwe na matokeo chanya. 

“Tupo wengi ndani ya chama na wengine wazito kuliko mimi lakini mliona mimi ndiye nichukue nafasi baada ya kifo cha Mwalimu na Kiongozi wetu Hayati Maalim Seif Sharif Hamad niseme wazi nitajitahidi kwa kila njia kuhakikisha siwaangushi.
Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud akisalimiana na viongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.

"Nakumbuma alikuja Katibu na Makamu Mwenyekiti kuniambia natakiwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais niliwajibu hivi mnajua mimi ni fundi Seremala hivyo fundi Uwashi sitoweza wakanijibu kuwa naweza hivyo kwa maslahi ya chama nilikubali na kazi zinaendelea,” amesisitiza.  

Masoud amesema kukubali nafasi hiyo ilikuwa mtihani mzito ila anaamini waliomuana waliona uwezo wake hivyo akasisitiza ushirikiano ndani ya chama na serikali ili kuchochea maendeleo na mshikamano.
Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (SUK), Masoud Othman Masoud akisalimia wna kuzungumza na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo alipowasili kwenye Hoteli ya Lamada kushiriki Kikao cha Kamati Kuu ya Kawaida kinachofanyaka hotelini hapa leo.

Aidha, Masoud amewataka wana ACT kutosista kumrekebisha iwapo wataona anapotoka kwa kuwa hakuna mtu mkamilifu. 

Makamu wa Rais huyo amesema anashukuru chama chake kumpitisha katika nafasi hiyo ya ujumbe wa kamati kuu kwani atakuwa amekamilisha utekelezaji wa majukumu yake kwa sasa. 

Masoud amesisitiza mshikamano kwa viongozi na wanachama ili kuchochea maendeleo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news