NA MWANDISHI DIRAMAKINI
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kikamilifu kusimamia maadili, uwajibikaji na utawala wa sheria katika kuinua uchumi wa viwanda.
Sambamba na maendeleo ya watu kama ilivyoelezwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa wa miaka mitano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akihutubia kwenye Hafla ya nne ya ufunguzi wa Mtandao wa Sala na Maombi ya Kitaifa na Kimataifa katika Ukumbi wa Morena jijini Dodoma leo Juni 12,2021.
Dkt. Philip Isdor Mpango ameyabainisha hayo leo Juni 12, 2021 wakati akihutubia kwenye Hafla ya Nne ya Ufunguzi wa Mtandao wa Sala na Maombi ya Kitaifa na Kimataifa katika Ukumbi wa Morena jijini Dodoma.
Makamu wa Rais amesema kuwa, Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini katika kuhakikisha kuwa taifa linakuwa na ustawi bora kwa watu wake.
Pia amesema kuwa,Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa, maombi hayo ni kiunganisho baina ya wanadamu na Mungu wao na kama watoto wa Mungu katika kupendana na kuwajibika katika kuwatumikia watu wake.
Awali Mratibu wa Mtandao huo wa Maombi ya Kidunia, Dkt.Fredrick Ringo amesema kuwa, maombi hayo yamelenga kuombea viongozi wakuu wa serikali na taaisisi zake vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama.
Sambamba na Bunge na Mahakama ili vyombo hivyo viweze kutunga sheria bora kwa watu wake na mahakama kutoa haki kwa kila mtu.
Aidha, maombi hayo yamehudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wakiwemo viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, wakiwemo wabunge wa Bunge la Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wa serikali na vyama vya siasa,huku kauli mbiu ya maombi ikiwa “Utawala Bora,Uwajibikaji na Uongozi".
Tags
Habari